Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 2 2025-04-08

Name

Amb. Liberata Rutageruka Mulamula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Primary Question

MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kitongoji cha Kakoni - Misenyi ili iweze kuhudumia wananchi wa Kitongoji hicho na jirani?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea na ujenzi wa zahanati katika vijiji na mitaa inayokidhi vigezo ili kusogeza huduma za afya ya msingi karibu na wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2020/2021 hadi 2024/2025, Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi imepelekewa jumla ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati nane.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na mwongozo wa Serikali wa Ujenzi wa Vituo vya kutolea Huduma za Afya ngazi ya msingi unaelekeza ujenzi wa zahanati kwenye ngazi ya kijiji. Aidha, Kakoni ni miongoni mwa Kitongoji katika Kijiji cha Kitobo ambacho tayari kina zahanati. Hivyo, kwa mujibu wa mwongozo, Kitongoji cha Kakoni kitahudumiwa na Zahanati ya Kitobo. Ahsante.