Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Amb. Liberata Rutageruka Mulamula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Primary Question
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kitongoji cha Kakoni - Misenyi ili iweze kuhudumia wananchi wa Kitongoji hicho na jirani?
Supplementary Question 1
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na jibu zuri la Mheshimiwa Naibu Waziri, kitu ambacho nilitaka kujua ni kwamba, ni lini kituo kidogo cha afya kilichopo katika hicho Kitongoji kitaweza kuongezewa hadhi kuwa zahanati kwa maana ni kituo ambacho kitahudumia karibu vitongoji nane vya Kakoni, Musibuka, Luweru, Lushasha, Nyabutaizi na vingine vingi kwa sababu kile ulichokitaja kiko mbali sana? Ahsante sana.
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Sera ya Huduma za Afya Msingi, ujenzi wa zahanati unafanyika kwenye kijiji kinachokidhi vigezo, lakini pia kwenye mitaa ambayo inakidhi vigezo. Kwa hiyo, kwa sababu tayari katika Kijiji hiki cha Kitobo tayari kuna zahanati, naomba tu nitumie nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kwamba tutaendelea kufanya tathmini kuona umbali wa Kitongoji hicho cha Kakoni ambacho kiko ndani ya Kijiji cha Kitobo na ikiwa kutakuwa na ulazima wa kujenga zahanati, basi tutawasiliana na halmashauri ili taratibu zianze. Hata hivyo, kwa sasa kwa mujibu wa Sera, kitongojii hicho kitapata huduma ndani ya Kijiji cha Kitobo. Ahsante sana.
 
											Name
Esther Edwin Maleko
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kitongoji cha Kakoni - Misenyi ili iweze kuhudumia wananchi wa Kitongoji hicho na jirani?
Supplementary Question 2
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itajenga Wodi ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya Funvuhu iliyopo kwenye Kata ya Old Moshi Mashariki, kwa sababu iliyopo kwa sasa haikidhi vigezo? Ninashukuru. (Makofi)
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya tathmini na kuainisha zahanati zote na hususani zahanati zile zilizojengwa miaka 20 iliyopita, ambazo majengo yake yalikuwa madogo na yalikuwa hayana chumba kikubwa kinachotosheleza huduma za uzazi (Wodi ya Wazazi). Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, hiyo zahanati tutaiingiza kwenye mpango wa kupanua ili kupata jengo kwa ajili ya mama wajawazito kupata chumba cha kujifungulia na kuboresha zaidi huduma za afya katika eneo hilo. Ahsante sana.
 
											Name
Aida Joseph Khenani
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kitongoji cha Kakoni - Misenyi ili iweze kuhudumia wananchi wa Kitongoji hicho na jirani?
Supplementary Question 3
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Runyala, Kanazi na Kakoma viko mbali na Hospitali ya Wilaya, hawana Vituo vya Afya na wamekwishaanza jitihada za kujenga zahanati. Ni mkakati upi wa Serikali wa kupeleka fedha ili kuweza kujenga zahanati hizo? Ninakushukuru.
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, kufanya tathmini katika vijiji hivyo vya Kanazi na hivyo vijiji vingine ambavyo Mheshimiwa Mbunge amevitaja. Pia, ikiwa vinakidhi vigezo vya kujengewa zahanati, halmashauri ianze kukusanya mapato ya ndani kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kushirikiana na nguvu za wananchi. Vilevile na sisi Serikali Kuu tutaanza kuweka kwenye mpango wa bajeti kwa awamu ili kujenga zahanati hizo na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi hao. Ahsante sana.
 
											Name
Selemani Moshi Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tanganyika
Primary Question
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Zahanati Kitongoji cha Kakoni - Misenyi ili iweze kuhudumia wananchi wa Kitongoji hicho na jirani?
Supplementary Question 4
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Serikali imeleta vifaatiba kama vile X- ray na Ultrasound kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika na vituo vyote vya afya na hatuna mtaalam kwenye eneo hilo; je, ni lini Serikali italeta mtaalam wa mionzi ili aweze kufanya kazi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika pamoja na vituo vya afya?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Ni kweli kwamba Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeweka kipaumbele cha hali ya juu sana katika upatikanaji wa vifaatiba vya kisasa katika zahanati na hospitali zetu zote za halmashauri. 
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Halmashauri ya Tanganyika imepata vifaatiba vya kutosha ikiwemo digital x-ray. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kwa kushirikiana na wadau, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Wizara ya Afya, tumeanzisha programu maalum ya mafunzo ya muda mfupi ya wataalam wa X- Ray na Ultrasound na mara watakapokuwa wamehitimu tutawapeleka kwenye vituo vyetu vyote vyenye upungufu ikiwemo Kituo cha Afya katika Halmashauri hiyo ya Tanganyika.  Ahsante sana.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved