Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 3 2025-04-08

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza:-

Je, lini fedha za ujenzi wa Majengo ya X-ray, OPD, Wodi za Wagonjwa, Mortuary, Kuchomea Taka, kufulia na Walk ways zitapelekwa Vituo vya Afya vya Kondoa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya nchini, ambapo katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 shilingi bilioni 107 zimetolewa na kujenga vituo vya afya 367 kote nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua uwepo wa upungufu wa miundombinu katika Vituo vya Afya vya Serya, Kolo na Kingale vilivyopo katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa. Kituo cha Afya Serya kina upungufu wa miundombinu ya wodi za kulaza wagonjwa, jengo la mionzi pamoja na jengo la kuhifadhia maiti. Kituo cha Afya Kolo hakina jengo la kufulia, jengo la mionzi, njia za kutembelea wagonjwa na kichomea taka. Pia, Kituo cha Afya Kingale hakina jengo la mionzi, njia za kutembelea wagonjwa pamoja na wodi za kulaza wagonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukamilishaji wa miundombinu ya majengo haya katika vituo vyetu vya afya, itaendelea kufanyika kwa awamu kote nchini vikiwemo Vituo vya Afya Kolo, Kingale na Mongoroma katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa. Ahsante.