Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 4 2025-04-08

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza:-

Je, lini Serikali itavipatia Magari ya kubebea wagonjwa Vituo vya Afya vya Magazini na Lusewa – Namtumbo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika Mwaka wa Fedha 2021/2022 ilinunua magari 594 ya kubebea wagonjwa na usimamizi wa huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, magari haya yamesambazwa kwenye Halmashauri kwa wastani wa magari mawili hadi manne kwa kila Halmashauri, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo imepokea magari mawili ya kubebea wagonjwa. Magari hayo yanatumika katika Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo na Kituo cha Afya cha Mtakanini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutekeleza mipango ya kununua magari ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya vituo vya afya nchini vikiwemo Vituo vya Afya vya Magazini na Lusewa – Namtumbo. Ahsante.