Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Vita Rashid Kawawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Namtumbo
Primary Question
MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza:- Je, lini Serikali itavipatia Magari ya kubebea wagonjwa Vituo vya Afya vya Magazini na Lusewa – Namtumbo?
Supplementary Question 1
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Vituo hivi vya Afya viwili, kimoja cha Magazini kiko kilometa 254 mpaka kufikia Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya na hiki cha Lusewa kiko kilometa 220 mpaka kufikia Makao Makuu ya Wilaya. Vilevile, kuna kingine cha Ligela kiko kilometa 110. Je, Serikali iko tayari kutuletea hayo magari ya vituo vya afya vilivyo mbali kabisa na makao makuu ya Wilaya?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa Kata za Kimkakati za Namabengo, Mgombasi na Mchomolo nazo zina uhitaji wa vituo vya afya. Pia, Mheshimiwa Rais alipopita Namtumbo tarehe 27 mwezi Septemba, wananchi wa Mchomolo walimwomba kituo cha afya eneo hilo…
NAIBU SPIKA:  Mheshimiwa, twende kwenye swali.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Waziri wa TAMISEMI, alikubali. Je, ni lini watawaletea fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mchomolo?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kama ambavyo Serikali imepeleka magari ya wagonjwa mawili katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, tunatambua pia uhitaji wa magari hayo katika Kituo cha Afya cha Magazini na Lusewa. 
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, safari ni hatua na tunakwenda kwa awamu. Tumepeleka magari mawili mapya ndani ya miaka miwili. Vilevile, tutahakikisha pia tunapotenga bajeti nyingine kwa ajili ya magari ya wagonjwa, tutatoa kipaumbele kwenye vituo hivi vya afya ambavyo viko mbali sana kutoka Hospitali ya Halmashauri.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili; maelekezo ya Mheshimiwa Rais ni kipaumbele namba moja kwenye utekelezaji wa bajeti zetu. Pia, tunafahamu kwamba ni maelekezo yake kuwa tupeleke Kituo cha Afya Kata ya Mchomolo. Pia, nimhakikishie Mbunge tayari tumeingiza kwenye Mpango wa Bajeti mwaka 2025/2026 kupitia World Bank ili kuhakikisha Kituo hicho cha Afya kinajengwa pale Mchomolo.  Ahsante.
							
 
											Name
Jonas Van Zeeland
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza:- Je, lini Serikali itavipatia Magari ya kubebea wagonjwa Vituo vya Afya vya Magazini na Lusewa – Namtumbo?
Supplementary Question 2
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Naibu Spika, Vituo vya Afya vya Mziha, Mvomero, Melela na Mlali, hawana magari ya kubebea wagonjwa. Je, lini Serikali itapeleka magari ya kubeba wagonjwa katika vituo hivi? Ahsante.
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba, Serikali inapeleka magari ya wagonjwa katika vituo vya afya na hospitali za halmashauri. Hata hivyo, kwenye vituo vya afya si kila kituo cha afya lazima kiwe na gari la wagonjwa. Kwa sababu, Kituo cha afya kimoja kinaweza kikawa na satellite facilities tatu au nne kwa ajili ya kutumia lile gari moja la wagonjwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Jonas, kwamba tumepokea mahitaji hayo ya vituo hivyo vya afya kupata magari ya wagonjwa na tutakwenda kuyafanyia kazi ili kuona angalau kimoja au viwili ambavyo vinaweza vikahitaji gari la wagonjwa mbali na vituo vyote ambavyo Mheshimiwa Mbunge amevitaja.  Ahsante.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved