Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 5 2025-04-08

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa zahanati iliyoboreshwa ya Mangio iliyopo Kata ya Mwaniko, Wilayani Mwanga?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Zahanati ya Mangio ilianzishwa kwa nguvu za wananchi mwaka 2010 na baadaye kuendelea kukamilishwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri, Serikali Kuu na Mfuko wa Jimbo ambapo jumla ya shilingi milioni 74 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo, ambapo kwa sasa iko 85% ya ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga imetenga shilingi milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Mangio. Ahsante.