Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa zahanati iliyoboreshwa ya Mangio iliyopo Kata ya Mwaniko, Wilayani Mwanga?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali na ahadi hiyo ya kutenga fedha za halmashauri, ninaomba tu niulize swali moja. Kwa kuwa Halmashauri ya Mwanga ni moja kati ya halmashauri zenye changamoto kubwa sana ya mapato. Je, Serikali haioni umuhimu wa kutoa upendeleo kwa zahanati hii ambayo imekuwa bila kukamilika kwa muda mrefu sana kiasi ambacho imeanza kuharibika sasa? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninafahamu na Mheshimiwa Mbunge ametolea hoja kuhusu Zahanati ya Mangio mara kadhaa na imechukua muda mrefu kukamilika tangu mwaka 2010 hadi sasa. Hata hivyo, nimhakikishie tu kwamba, kwa sababu tayari Serikali Kuu ilishapeleka fedha, lakini na yeye mwenyewe kupitia Mfuko wa Jimbo jumla ya milioni 74 na tayari halmashauri kwa Mwaka ujao wa Fedha 2025/2026 imetenga milioni 20. Tuna uhakika kwamba, katika mwaka huu wa fedha mapema, zahanati hii itakamilishwa na wananchi wataanza kupata huduma zilizokamilika katika ngazi ya zahanati. Ahsante.

Name

Michael Constantino Mwakamo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Vijijini

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa zahanati iliyoboreshwa ya Mangio iliyopo Kata ya Mwaniko, Wilayani Mwanga?

Supplementary Question 2

MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Pale kwenye Kijiji cha Ngwale kwenye Kata ya Gwata, wananchi wameanza ujenzi wa zahanati kwa nguvu zao. Je, ni lini Serikali itawaongezea nguvu ili waweze kukamilisha zahanati hiyo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninawapongeza wananchi wa Gwata kwa kuanza ujenzi wa zahanati kwa nguvu zao. Pia, kwa kadri ya mwongozo wakifika hatua ya lenta, tutahitaji taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ili iweze kuingizwa kwenye bajeti ya kupewa fedha ya ukamilishaji wa zahanati hiyo ya Gwata. Ahsante.

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa zahanati iliyoboreshwa ya Mangio iliyopo Kata ya Mwaniko, Wilayani Mwanga?

Supplementary Question 3

MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Nandwahi ambacho kipo Jimbo la Newala, wananchi waliwekeza fedha zao nyingi kwa ajili ya kukiboresha. Je, ni lini Serikali italeta fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo kile ili kurahisisha huduma za tiba kwa wananchi wa Jimbo la Newala Vijijini? Ninakushukuru.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Vijijini, kufanya tathmini ya gharama zinazohitajika kwa ajili ya ukamilishaji wa Kituo hicho cha afya na kuwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI, ikihusisha mpango wa mapato ya ndani kuchangia shughuli hiyo ya ujenzi. Vilevile, Serikali kuu itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hicho cha afya.