Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Planning and Investment Ofisi ya Rais: Mipango na Uwekezaji 6 2025-04-08

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:-

Je serikali ina mpango gani wa njia mbadala ya kukuza uchumi wa wananchi wa Hai kutokana na uhaba wa ardhi ya uzalishaji?

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Elinikyo Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali ili kuwawezesha wananchi kukua kiuchumi wakiwemo wananchi wa Wilaya ya Hai. Mikakati hiyo ni pamoja na:-

Kutoa Mikopo yenye riba nafuu hususan kwa wanawake, vijana na walemavu; Kujenga mfumo wa kidijitali vijijini ili kuongeza matumizi ya TEHAMA katika shughuli za kiuchumi; na Kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uwekezaji, hasa katika Sekta ya Viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Wilaya ya Hai, Serikali imeendelea kuhakikisha Mradi wa Kiwanda cha KMTC (Kilimanjaro Machine Tools Company) ambacho kiko chini ya NDC unatekelezwa. Aidha, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Hai imetenga eneo maalum la uwekezaji lenye ukubwa wa hekta 463 ambalo linaendelea kutangazwa kwa wawekezaji mbalimbali. Hivyo, Serikali itaendelea kuhimiza na kutangaza fursa zinazopatikana katika Wilaya ya Hai ikiwemo fursa za Utalii ili kuimarisha uchumi wa wananchi. Ahsante sana.