Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:- Je serikali ina mpango gani wa njia mbadala ya kukuza uchumi wa wananchi wa Hai kutokana na uhaba wa ardhi ya uzalishaji?
Supplementary Question 1
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwa, sehemu kubwa ya ardhi ya Wilaya ya Hai, iko kwenye mashamba 17 yaliyoko kwenye vyama vya ushirika. Je, Serikali haioni iko haja ya kufanya tathmini ya ardhi ya mashamba haya yote 17 ili tunapoingia mikataba, tuingie mikataba tukihusianisha na thamani ya ardhi tulionayo?  
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; moja ya sababu inayosababisha kufifisha uchumi wa Jimbo la Hai ni wawekezaji wasio na uwezo wanaoingia mikataba kwenye mashamba haya ya ushirika. Kwa mfano, shamba la Makoa, Kijiji cha Uduru ni miaka minne shamba lile limesimama, mwekezaji halipi chochote, mwekezaji ni migogoro kila siku ni Mahakamani na wanachi wanakosa uchumi kwenye shamba hilo. Shamba la Mrososangu mwekezaji ameingia mkataba ajenge kiwanda cha parachichi mpaka sasa hivi hajafanya. 
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa twende kwenye swali, najua kuna presha ya uchaguzi, twende kwenye swali. (Kicheko)
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE:  Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali haioni haja ya kuingilia migogoro hii iliyopo kwenye mashamba ya ushirika ili uchumi wa Jimbo la Hai ambao unategemea kwa kiwango kikubwa sana haya mashamba 17? Ahsante.
 
											Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Saashisha kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru na nimpongeze kwa kweli amekuwa ni championi mkubwa anayefuatilia masuala ya ushirika katika wilaya yake na kwa kweli ni Mbunge ambaye yuko makini nashukuru sana kwa hilo nampongeza. 
Mheshimiwa Naibu Spika, mashamba 17 yaliyoko chini ya ushirika ikiwa ni pamoja na hayo mashamba ambayo yako chini ya mkataba wa huyu mwekezaji, Ofisi ya Rais masuala ya uwekezaji, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, katika bajeti inayofuata ya mwaka huu tumeweka mkakati mkubwa ambao tutakwenda kufanya tathmini ya mali zote ambazo ziko chini ya TR na mali zote ambazo ni za Serikali, kuzifanyia tathmini ya kina kujua thamani ili tunapoingia mikataba ya uwekezaji tuweze kujua tunaingia mikataba katika ardhi au mali ya Serikali yenye thamani ipi. 
Mheshimiwa Naibu Spika, huo mkakati upo, Bunge likitupitishia bajeti tutakwenda kufanya kazi hiyo ya tathmini na hii itakuwa ni hatua moja nzuri sana ya kuweza ku-move mbele kuweza kuangalia namna ya kuingia mikataba ambayo ni yenye tija, mikataba ambayo inakuwa na manufaa na Serikali. Kwa hiyo, nimtulize Mheshimiwa Mbunge atulie tunakwenda kufanya hiyo kazi. 
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kwa hizi kesi ambazo ziko mahakamani ninasita kuongea kwa sababu ziko mahakamani, basi ni vizuri kuchukua hatua stahiki ili tuweze kuona ni namna gani ya kuweza kwenda mbele katika kuleta tija pande zote mbili kati ya mwekezaji pamoja na wananchi wa Hai. Ahsante sana.
							
 
											Name
Yustina Arcadius Rahhi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:- Je serikali ina mpango gani wa njia mbadala ya kukuza uchumi wa wananchi wa Hai kutokana na uhaba wa ardhi ya uzalishaji?
Supplementary Question 2
MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kutangaza fursa nyingi za uwekezaji zilizoko Mkoani Manyara, ikiwa ni pamoja na kilimo cha ngano?
 
											Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, msingi wa majibu yangu ni ule ule kwamba tunakwenda kufanya tathmini kubwa ya mali zote za Serikali yakiwemo mashamba, vilevile kwa kushirikiana na Sekretarieti za Mkoa pamoja na Sekretarieti za Wilaya kuangalia namna ya kuweza kuonesha fursa za uwekezaji katika maeneo hayo. Tutakwenda kutafuta wawekezaji wa ndani na nje kuwawekea mazingira mazuri ya kuwekeza katika fursa tofauti tofauti katika mikoa yetu ambayo iko chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu kabisa kila mkoa una fursa zake za kiuwekezaji, ni namna bora tu ya kukaa na kuangalia ni fursa zipi tuwape wawekezaji ili waweze kuwekeza na wananchi wa maeneo hayo waweze kupata tija katika uwekezaji huo.
							
 
											Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:- Je serikali ina mpango gani wa njia mbadala ya kukuza uchumi wa wananchi wa Hai kutokana na uhaba wa ardhi ya uzalishaji?
Supplementary Question 3
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Kyerwa kutokana na uoto wa asili na ardhi yake ina fursa nyingi za kibiashara, lakini inabaki kuwa maskini. Ninataka nijue mkakati wa Serikali kwa kutumia Mto Kagera ili wananchi waweze kuwekeza kwenye vizimba, iweze kusaidia kuongeza uchumi, kipato cha wananchi, uwezo, nia na nguvu wanaweza kufanya hivyo? Ninakushukuru.
 
											Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anatropia kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali yetu tumekuwa sasa katika utaratibu wa kuandaa dira ya mwaka 2050 baada ya kumaliza dira ya mwaka 2025 ambayo inakwisha mwakani yaani bajeti hii tunayokaa ni bajeti ya mwisho. Naomba nikuhakikishie tumeweza ku-identify na kuangalia kwa kupitia ushauri wa wananchi, tumeweza kuangalia namna ya kwenda kuziwezesha zile sekta ambazo ni za kimkakati ambazo zitakwenda kusaidia kutengeneza na kuongeza uchumi wa nchi yetu, wakati huo huo kutengeneza fursa za ajira kwa wananchi wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya maeneo ni ya kilimo, uchumi wa bluu na haya yote yanakwenda kufanyiwa kazi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunayo mikakati mizuri ya kuhakikisha kila sekta ambayo tunaona ina tija katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu, ikiwemo masuala ya kilimo na mambo mengi, tunakwenda kuyafanyia kazi vizuri na fursa zitakwenda kufunguka za kutosha.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved