Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 7 2025-04-08

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE K.n.y. MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza:-

Je, lini umeme utapelekwa katika eneo la Kitame, Kata ya Makurunge ili kuwasaidia wazalishaji wa chumvi?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Wilaya ya Bagamoyo, Serikali kupitia REA inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme kwenye maeneo ya migodi midogo yakiwemo maeneo ya wazalishaji wa chumvi kupitia mkandarasi aitwaye Dieynem Company Limited. Hadi kufikia mwezi Machi 2025, jumla ya maeneo 14 ya migodi midogo imepelekewa umeme ambapo kati ya hayo, maeneo matatu ni ya wachimbaji wa chumvi wanaopatikana katika eneo la Kitame Kata ya Makurunge, ambapo jumla ya wachimbaji 34 wanaopatikana katika maeneo hayo wamefikiwa na huduma ya umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi ya kupeleka umeme kwa wachimbaji wa chumvi waliosalia itaendelea kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.