Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Primary Question

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE K.n.y. MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza:- Je, lini umeme utapelekwa katika eneo la Kitame, Kata ya Makurunge ili kuwasaidia wazalishaji wa chumvi?

Supplementary Question 1

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na jitihada kubwa zilizofanyika kuweza kupeleka umeme kwa wachimbaji wa migodi wale wadogo wadogo lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali ina mkakati gani wa kuweza kupeleka umeme kwenye Kitongoji cha Kitame ili wananchi waweze kunufaika katika nyumba zao?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; zaidi ya shilingi bilioni 3.8 zimetumika pale katika Jimbo la Kibiti kupeleka umeme katika zile Kata Delta, Kata ya Kiongoroni, Mbuchi, Maparoni na Msala. Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kibiti naomba Mheshimiwa Waziri tufikishie salamu zetu na pongezi kwa Mheshimiwa Rais ili alivyoweza kufanikisha ndoto za wanakibiti wanaoishi katika maeneo ya Delta kuweza kupata umeme.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Katika eneo hili la Kitame tunayo miradi ya vitongoji ambayo inafuata, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba wananchi wa Kitongoji hiki na wenyewe watanufaika na huduma hiyo ya umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapokea salamu za Mheshimiwa Mbunge kwa kweli ni pongezi kwa Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa inayofanyika katika Sekta ya Nishati ambayo inasimamiwa vizuri sana na Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko. Ahsante.

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE K.n.y. MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza:- Je, lini umeme utapelekwa katika eneo la Kitame, Kata ya Makurunge ili kuwasaidia wazalishaji wa chumvi?

Supplementary Question 2

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama kituo cha kupoozea umeme kilichoko eneo la Uhuru Wilaya ya Urambo kimekamilika, je, ni lini kituo hicho kitazinduliwa rasmi? Ahsante. (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tarehe 26 Machi, tuliwasha kituo cha kupooza umeme cha Uhuru Substation na kwa sasa hivi wananchi wananufaika kupitia feeder ambazo tumezipeleka katika maeneo ya Kaliua pamoja na Urambo.

Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu amesikia ombi la Mheshimiwa Mbunge na kwa hiyo nina uhakika tutaweza kulichakata na kulifanyia kazi. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE K.n.y. MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza:- Je, lini umeme utapelekwa katika eneo la Kitame, Kata ya Makurunge ili kuwasaidia wazalishaji wa chumvi?

Supplementary Question 3

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, lini mchakato wa umeme katika vitongoji 15 utaanza, ukizingatia katika Jimbo la Kilombero kumekuwa na uhaba mkubwa sana wa umeme katika Kata ya Michenga, Vitongoji vya Tupendane na Upendo? Ahsante sana.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, mkandarasi wa kupeleka umeme katika vitongoji 15 katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge ameshapatikana na ameshaanza kazi katika maeneo mengine. Tunaendelea kumsisitiza mkandarasi aongeze magenge na aongeze nguvu ili kuweza kufikia Majimbo mengine katika Mkoa wa Morogoro. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kumsimamia mkandarasi huyo ambaye ameanza katika maeneo mengine kwa kadri ya maelekezo ya RCC ambayo walikuwa wamekubaliana na baada ya hapo atafika kwenye Jimbo la Mheshimiwa Mbunge. Ahsante. (Makofi)