Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 8 2025-04-08

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Primary Question

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Miradi ya Umwagiliaji ya Udima na Mbwasa – Manyoni?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya umwagiliaji nchini zikiwemo Skimu za umwagiliaji za Udimaa na Mbwasa zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa Skimu za Udimaa na Mbwasa kwa ajili ya ujenzi. Taratibu za manunuzi kwa ajili ya ujenzi wa Skimu ya Mbwasa umekamilika mwezi Februari, 2025 na mkandarasi amekabidhiwa eneo la mradi. Aidha, Skimu ya Udimaa ilitangazwa kwa ajili ya kupata mkandarasi ila taratibu za manunuzi hazikukamilika. Skimu hiyo imetangazwa tena ili kumpata mkandarasi ambaye atakamilisha ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kukamilika kwa miradi hii kutanufaisha wakazi zaidi ya 13,000 wa Vijiji vya Kintinku, Mbwasa, Mwiboo, Chikuyu, Chilejeho na Mtiwe vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni. Ahsante sana.