Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Dr. Pius Stephen Chaya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni
Primary Question
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Miradi ya Umwagiliaji ya Udima na Mbwasa – Manyoni?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; katika Kata ya Sanza iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kuna mto mkubwa ambao unamwaga maji kwenye vijiji vinne na ni potential kwa kilimo cha umwagiliaji. Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba wanaanzisha Skimu ya Umwagiliaji katika Kata ya Sanza?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; katika Kata ya Makulu iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, kuna Skimu ya Umwagiliaji ya Msemembo ambayo imeharibika ndani ya miaka mitatu. Sasa nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunawanusuru wakulima hao? Ahsante sana.
 
											Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
								NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge, Dkt. Pius Chaya kwa kufanya kazi nzuri kwa wananchi wa Jimbo la Manyoni Mashariki. Jambo moja ambalo nimthibitishie ni kwamba, katika huu mkakati wa kuanzisha Skimu ya Umwagiliaji katika Kata ya Sanza tuko katika hatua ya upembuzi yakinifu. Kwa hiyo, tunaendelea kufanya baada ya hapo tutatangaza mkandarasi ili aweze kupatikana na kutekeleza mradi huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu marekebisho kwenye mradi ya Msemembo hayo yapo katika mpango wetu na katika kila mwaka wa fedha tunatenga fedha kwa ajili ya ukarabati. Kwa hiyo na jambo hilo vilevile tutalitekeleza.  Ahsante sana. (Makofi)
							
 
											Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Miradi ya Umwagiliaji ya Udima na Mbwasa – Manyoni?
Supplementary Question 2
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Isebya na Kata ya Bugerenga Wilayani Bukombe miradi hii miwili haijapatiwa fedha.  Je, ni lini Serikali itatoa fedha ili miradi hii iweze kutengenezwa na wananchi waweze kupata manufaa?
NAIBU SPIKA: Hebu rudia tena swali lako.
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Isebya inayo Mradi wa Skimu na Kata ya Bungerenga, lakini miradi haifanyi kazi.  Je, ni lini Serikali itatoa fedha ili miradi hii ianze kufanya kazi?  Ahsante. (Makofi)
 
											Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli anachokisema Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika Miradi miwili aliyoitaja ikiwemo ya Isebya na Bungerenga ambayo bado hatujapeleka fedha, tayari Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tumeomba fedha Wizara ya Fedha ambayo wameahidi kutukamilishia kati ya mwezi huu Aprili na mwezi Mei. Kwa hiyo, fedha hizo zitakapofika maana yake tutapeleka ili ile miradi iendelee kutekelezwa. Ahsante.
 
											Name
Salma Rashid Kikwete
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mchinga
Primary Question
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Miradi ya Umwagiliaji ya Udima na Mbwasa – Manyoni?
Supplementary Question 3
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kilimo cha umwagiliaji ni muhimu sana katika ustawi wa chakula katika Taifa letu la Tanzania. Je, kutokana na skimu za umwagiliaji ambazo zinaleta tija, sisi tunalo Bonde la Kinyope, ni lini fedha zitapelekwa ili tuweze kuanza hiyo kazi, kwa sababu bonde hili lina watu wengi zaidi ya 25,000? Ahsante sana.
 
											Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mama Salma Kikwete Mbunge wa Jimbo la Mchinga kwamba, moja ya kazi kubwa ambayo Wizara ya Kilimo tunaifanya sasa ni kufanya usanifu wa kina katika mabonde yote ikiwemo Bonde la Kinyope, baada ya kukamilika kwa bonde hili maana yake tutatafuta fedha ili ziweze kupelekwa pale na ujenzi uanze kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Jimbo la Mchinga. Ahsante.
 
											Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Miradi ya Umwagiliaji ya Udima na Mbwasa – Manyoni?
Supplementary Question 4
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Kilimo kupitia eneo la umwagiliaji wamefanya upembuzi wa kina kuhusiana na ujenzi wa Bwawa kubwa la Lunguya katika Kata ya Talaga na tulitarajia kwamba zoezi la ujenzi lingeanza kabla ya mwaka wa fedha haujakwisha. Je, Serikali inasema nini kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo kwa ajili ya kilimo cha mpunga? Nakushukuru sana. (Makofi)
 
											Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba, katika Bonde la Lunguya lililopo katika Jimbo la Kishapu ni kweli Wizara tunalifahamu na tunafanyia kazi. Jukumu kubwa ambalo tulilonalo sasa hivi ni zile fedha ambazo tumeomba Wizara ya Fedha, tukishapata zile fedha maana yake tutapeleka katika maeneo yote ambayo yamepangwa kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha. Kwa hiyo, bonde lako pia liko katika mpango huo. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved