Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Water and Irrigation Wizara ya Maji 9 2025-04-08

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Mradi wa Maji Kata ya Matemanga katika Vijiji vya Milonde, Matemanga na Changarawe – Tunduru?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Vijiji vya Milonde, Matemanga na Changarawe vilivyopo Kata ya Matemanga Wilayani Tunduru vinapata huduma ya majisafi na salama kupitia vyanzo vya maji vya Mkwinda na Namalowe. Mradi huo ulijengwa mwaka 1980 na baadaye kwa nyakati tofauti kufanyiwa ukarabati katika vipindi viwili tofauti vya mwaka 2012 na 2021 ili kuboresha ufanisi katika utoaji wa huduma wa skimu hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya ongezeko la mahitaji ya huduma ya maji kwa wananchi wa Kata ya Matemanga kutokana na ongezeko la idadi ya watu ambapo kwa sasa imefikia zaidi ya watu 10,000. Serikali katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, itajenga tanki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 500,000 ili kuongeza uzalishaji kutoka lita 275,000 za sasa kwa siku na kufikia lita 775,000. Lengo ni kuhakikisha wananchi wa Kata ya Matemanga wanapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza.