Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Mradi wa Maji Kata ya Matemanga katika Vijiji vya Milonde, Matemanga na Changarawe – Tunduru?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo majibu aliyatoa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.  Swali la kwanza; je, ni lini ahadi ya maji aliyoitoa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa mwaka 2017 itatekelezwa katika Kata Kalulu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; wananchi wa Kata ya Maposeni ikiwemo Kijiji cha Mdunduwaro wana hamu sana ya kupata maji. Je, ni lini sasa mradi huo utakamilika?  Ninakushukuru. (Makofi)
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali ya nyongeza yaliyoulizwa na Mheshimiwa Dkt. Ntara kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa upande wa Tunduru Kaskazini Serikali inaendeleza miradi saba, miradi yenye gharama ya bilioni 2.146, katika miradi hiyo miradi miwili imeshakamilika. Tunatambua kwamba, ahadi za viongozi wa kitaifa inaendelea kutekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha na mradi huu kwa Wizara ya Maji ni kipaumbele, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba huu mradi ni kipaumbele katika Sekta yetu ya Maji kuhakikisha kwamba unakamilika. 
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile katika eneo la Mdunduwaro ambalo liko katika eneo la Songea tayari tulishapata Mkandarasi na tunaamini kwamba bado yuko ndani ya mkataba wa utekelezaji wake, nimwombe tu Mheshimiwa Mbunge awe na subira kidogo, mradi huu utakamilika na utatoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wake.  Ahsante sana. (Makofi)
							
 
											Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Mradi wa Maji Kata ya Matemanga katika Vijiji vya Milonde, Matemanga na Changarawe – Tunduru?
Supplementary Question 2
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Serikali imefanya kazi nzuri sana ya kupeleka mradi wa maji Kijiji cha Hunyari kwa shilingi milioni 830, lakini mpaka leo wananchi wa Hunyari wanapata shida juu suala la maji. Je, ni lini Serikali itakamilisha huu mradi? (Makofi)
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Getere kwa kazi kubwa anayoifanya kwa wananchi wake. Pili, nampongeza kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwemo kupeleka fedha ambazo ni shilingi milioni 830 katika eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelitaja.
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo alilolitaja, changamoto iliyopo pale ni pampu ambayo ilikuwa inatumika kusukuma maji, bado inadaiwa kiasi cha shilingi milioni mia mbili na thelathini na kitu, ambapo Wizara ya Maji imeishapokea na inalifanyia kazi. Litakapokamilika, huduma ya maji itaanza kutoka katika eneo hilo bila kuwa na shaka yoyote, ahsante sana.
							
 
											Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Mradi wa Maji Kata ya Matemanga katika Vijiji vya Milonde, Matemanga na Changarawe – Tunduru?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Mradi wa Kata ya Boma la Ng’ombe utakamilika kwa sababu, wananchi wa kata hiyo wamekuwa wakiusubiri kwa muda mrefu, ili kumtua mwanamke ndoo kichwani na kupata maji safi na salama? (Makofi)
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge kutoka Mkoa wa Iringa. Eneo la Boma la Ng’ombe, tayari Serikali imeishapeleka fedha na mradi huu umeshaanza kujengwa na tumeshakamilisha tenki na sasa kazi iliyobaki ni kuunganisha huduma ya nishati ya umeme ili sasa zile pampu ziweze kuanza kusuma maji. Wananchi ambao Mheshimiwa Ritta Kabati anaendelea kuwapigania, basi watapata huduma ya maji safi na salama, ili waweze kuendelea kushuhudia makubwa yanayofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved