Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Water and Irrigation Wizara ya Maji 10 2025-04-08

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:-

Je, lini Wananchi wa Kijiji cha Sambaru, Kata ya Mang'onyi, Singida Mashariki, watapata maji safi na salama?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Sambaru kilichopo Kata ya Mang’onyi, Wilayani Ikungi, kinapata huduma ya maji safi na salama kupitia Skimu ya Maji ya Sambaru iliyojengwa mwaka 2003, kwa ajili ya kuhudumia watu 4,048 wa kijiji hicho. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, kijiji hicho kinakadiriwa kuwa na watu 6,830, hivyo kuwa na ongezeko la mahitaji ya maji ukilinganisha na huduma inayotolewa kupitia miundombinu iliyopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia mwezi Februari, 2025, Serikali imekamilisha uchimbaji wa kisima kirefu chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 2,800 kwa saa. Aidha, kwa sasa zoezi la ujenzi wa point source ya kutolea huduma kwa wananchi linaendelea. Sambamba na hilo, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali itatenga bajeti zaidi kwa ajili ya utafutaji wa vyanzo vya maji vya uhakika katika kijiji hicho kwa lengo la kuboresha huduma ya maji safi, salama na yenye kutosheleza, ahsante.