Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 1 | Home Affairs | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | 11 | 2025-04-08 | 
 
									Name
Saada Mansour Hussein
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
						MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN aliuliza:-
Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya Vituo vya Polisi na vitendea kazi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja?
					
 
									Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
						NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Kaskazini Unguja una wilaya mbili; za Kaskazini A na Kaskazini B, zenye jumla ya Vituo vya Polisi viwili Daraja A, Daraja B vituo vitatu, Daraja C kituo kimoja na kuna vituo viwili vya Polisi vya Tumbatu na Pwani Mchangani ambavyo vinaendelea na ujenzi. Mkoa huu una jumla ya magari ya Polisi 15 na pikipiki 22 zinazofanya kazi mbalimbali za Polisi. 
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Kaskazini A kuna magari matatu na pikipiki nane, na katika Wilaya ya Kaskazini B kuna magari mawili na pikipiki tisa. Serikali kupitia Halmashauri za Mji na Wilaya, zitaendelea kutoa maeneo kwa ajili ya kujenga Vituo vya Polisi, ikiwa ni pamoja na Serikali kutenga fedha toka kwenye Bajeti ya Serikali kila mwaka, kwa ajili ya kujenga Vituo vya Polisi na kununulia vitendea kazi kama magari na pikipiki, ili kutoa huduma bora kwa wananchi, ahsante. (Makofi)
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved