Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Saada Mansour Hussein
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya Vituo vya Polisi na vitendea kazi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja?
Supplementary Question 1
MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa maswali mawili ya nyongeza, na pia nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri. Swali langu la kwanza ni kwamba, Kituo cha Polisi Kiwengwa kina hali mbaya. Je, ni lini Serikali itakifanyia ukarabati kituo hiki? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Kwa kuwa, wananchi wa Vijiji vya Kichwele, Kichungwani, Muembe Majogoo, Mchanjarike na Kitopendani, wanatembea umbali mrefu kufuata Kituo cha Polisi Mahonda. Je, ni lini Serikali itawajengea Kituo cha Polisi? (Makofi)
 
											Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nampongeza Mheshimiwa Saada Monsour Hussein, Mbunge wa Viti Maalum kwa ufatiliaji wake makini. Kwa swali la kwanza kwamba Kituo cha Polisi alichokitaja hali yake ni mbaya; nimhakikishie kwamba, Serikali inafanya tathmini ya kuona uchakavu wa vituo vya Polisi na kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusu mahitaji ya Kituo cha Polisi kwenye eneo ambalo amelitaja, Serikali imetenga Ujenzi wa Vituo vya Polisi vya Kata na Shehia awamu kwa awamu. Kwa hiyo, nimhakikishie Mbunge kwamba kituo alichokitaja pia, kitawekwa kwenye mpango, tayari kwa ajili ya utekelezaji, ahsante. (Makofi)
							
 
											Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya Vituo vya Polisi na vitendea kazi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja?
Supplementary Question 2
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Je, lini Serikali itakamilisha Ujenzi wa Kituo cha Polisi katika eneo la Kizota, ambacho kimeanza kujengwa miaka miliwi na nusu iliyopita?
 
											Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, napongeza kazi iliyofanywa, na kituo kimefikia hatua nzuri. Niagize Jeshi la Polisi, kupitia, kufanya tathmini ya kiwango kilichofikiwa na kutenga fedha kwa ajili ya umaliziaji wa hiki Kituo cha Polisi cha Kizota, ahsante.
 
											Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya Vituo vya Polisi na vitendea kazi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja?
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Katika wilaya chache ambazo hazina Vituo vya Polisi ni pamoja na Wilaya ya Kalambo. Je, ni lini Serikali watajenga Kituo cha Polisi katika Wilaya ya Kalambo?
 
											Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kalambo. (Makofi)
 
											Name
Kunti Yusuph Majala
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza changamoto ya Vituo vya Polisi na vitendea kazi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja?
Supplementary Question 4
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Wilaya ya Chemba tumejengewa Kituo bora cha Polisi cha Wilaya, lakini hatujakamilisha ununuzi wa samani za ofisi. Ni lini Serikali itakamilisha ununuzi wa samani za ofisi ili ofisi ile ianze kutumika kwa ajili ya kuhudumia wananchi kama ilivyokusudiwa?
 
											Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Niwapongeze kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Chemba, ambacho kimekamilika. Nimhakikishie Mheshimiwa Kunti kwamba, katika mwaka wa fedha unaokuja 2025/2026, tutatenga fedha kwa ajili ya kununua samani ili kituo hicho kifanye kazi kama ambavyo imekusudiwa, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved