Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 12 2025-04-08

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. REGINA N. QWARAY K.n.y. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza gharama ya matibabu ya kusafisha figo katika hospitali zetu nchini?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imechukua hatua mbalimbali ili kupunguza gharama za kusafisha figo, ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma hizi kwa kuongeza vituo vya dialysis katika hospitali 15 za rufaa za mikoa, na hospitali zote za kanda nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, Serikali itaongeza wadau na taasisi zinazoingiza vitendanishi, vifaatiba na dawa zitumikazo badala ya kuacha mtu mmoja au taasisi kutawala soko bila kuruhusu ushindani na pia kuhamasisha viwanda na ubunifu ndani ya nchi. Aidha, Serikali imesambaza kwenye hospitali za rufaa za mikoa nchini mashine zaidi ya 100 pamoja na vitendanishi vyake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe rai kwa wananchi, mara utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote utakapoanza, waweze kujiunga, kwani ndiyo njia pekee ya kuweza kuwasaidia kuepukana na gharama za matibabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.