Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Regina Ndege Qwaray
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. REGINA N. QWARAY K.n.y. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza gharama ya matibabu ya kusafisha figo katika hospitali zetu nchini?
Supplementary Question 1
MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naishukuru sana Serikali kwa kutuletea huduma hii katika ngazi ya Mkoa na tayari Mkoa wa Manyara tumepokea vifaa, lakini pamoja na vifaa hivyo kufika ngazi ya mkoa kulingana na jiografia ya mkoa wetu, bado baadhi ya Wilaya zitakuwa katika umbali mrefu. Je, ni lini sasa Serikali itakwenda kusogeza huduma hizi katika ngazi za wilaya? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa, kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa ya figo. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwaandaa watalamu wa kutosha ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi waweze kuepukana na ugonjwa wa ufigo? (Makofi)
 
											Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
								NAIBU WAZIRI WA AFYA: Kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge Regina Ndege kwa jinsi ambavyo amekuwa akifuatilia masuala ya afya kwenye maeneo ya Mkoa wa Manyara. Amekuwa akifuatilia kwenye wilaya mbalimbali akishirikiana na Wabunge wa Majimbo husika.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu, maswali yake mawili ya msingi ni kwamba, sasa tumefika kwenye hospitali 15 za mikoa, tutaenda kumalizia hospitali zote kwa sababu kuna utaratibu wa kusomesha watalamu kupitia Mfuko wa Rais Samia Scholarship, na wataalamu watakapopatikana, basi tutawashusha. Watakapokuwepo wataalamu wenye uwezo ndani ya halmashauri zetu na kila Wilaya, sasa tutaanza kwenda pole pole na wilaya ziwezeshwe kufanya huduma kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameomba.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili juu ya suala la kutoa elimu, mimi nipokee, na kwa kweli kuna wataalamu. Sisi tutakachoongeza ni kwamba, hata kwenye kliniki, kila mahali ambapo elimu inatolewa kuhusu magonjwa mengine, tutahakikisha hatusahau kutoa elimu kuhusu matatizo ya figo. (Makofi)
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved