Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 1 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo | 13 | 2025-04-08 | 
 
									Name
Toufiq Salim Turky
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpendae
Primary Question
						MHE. AMINA ALI MZEE K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza:-
Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha ongezeko la vyombo vya habari mtandaoni haliathiri maadili na utamaduni wa Taifa letu?
					
 
									Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
						NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kutoa leseni za vyombo vya habari na waandaaji wa maudhui mtandaoni kwa maombi ambayo yanakidhi vigezo vilivyowekwa ili kupanua wigo wa kutoa habari nchini kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji. Hadi Machi, 2025, leseni 206 za televisheni na redio za mtandaoni zimetolewa. 
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia TCRA imeendelea kutoa elimu na imekuwa na programu maalumu za kuwaelimisha watumiaji wa mitandao kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao. Pia, kuendelea kufuatiilia wale wanaokiuka maadili ya Mtanzania na kuwawajibisha, ikiwemo kufungia uzalishaji wa maudhui na kuwapiga faini kwa mujibu wa Sheria za Vyombo vya Habari na za nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, mbali ya hayo, Serikali imeanzisha Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016. 
Mheshimiwa Naibu Spika, bodi hii inasimamia weledi na maadili kwa waandishi, na kuhakikisha waandishi wenye sifa tu ndio wanaoruhusiwa kutumika katika vyombo vya habari.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved