Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amina Ali Mzee

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha ongezeko la vyombo vya habari mtandaoni haliathiri maadili na utamaduni wa Taifa letu?

Supplementary Question 1

MHE. AMINA ALI MZEE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Kumekuwa na ongezeko kubwa la vyombo vya habari vya mtandaoni. Je, Bodi ya Ithibati inasimamiaje kuhakiki waandishi wa habari?

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA, NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, Bodi ya Ithibati lengo lake la msingi litakuwa ni kuhakikisha kwamba inasimamia weledi na maadili miongoni mwa waandishi wa habari, wakiwemo waandishi wa habari wa vyombo vinavyotekeleza majukumu yake mtandaoni. Itakuwa na jukumu la kusimamia vyote hivi ili kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanafanya shughuli zao kwa kufuata weledi, maadili, na kuzingatia usalama wa Taifa bila kukandamiza uhuru wa habari.