Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 14 2025-04-08

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaona haja ya kuwa na kiwanda cha asali Tarafa ya Kiwele – Sikonge?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Sikonge ina tarafa mbili ambazo ni Tarafa za Sikonge na Tarafa ya Kiwele. Serikali kupitia Mfuko wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services) ilijenga kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki Tarafa ya Sikonge. Kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata asali tani nne kwa siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kukidhi mahitaji ya kiwanda kilichojengwa, sasa Serikali itaanza mchakato wa awali wa kujenga kiwanda cha pili cha kuchakata mazao ya nyuki, ikiwa ni pamoja na kuainisha uwezo wa uzalishaji wa asali kwa Tarafa ya Kiwele. Ahsante.