Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini Serikali itaona haja ya kuwa na kiwanda cha asali Tarafa ya Kiwele – Sikonge?

Supplementary Question 1

MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Kama alivyosema, kuna kiwanda ambacho kimejengwa Wilaya ya Sikonge, lakini tangu kizinduliwe kiwanda kile hakijaanza kufanya kazi. Je, ni lini Serikali itaweza kuamua kiwanda hicho kiweze kufanya kazi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Kutoka Tarafa ya Kiwele kwenda Makao Makuu ya Wilaya ni takribani kilometa 300, na tarafa ile ina uzalishaji mkubwa sana wa asali. Je, Serikali haioni kuna haja kubwa ya kuweka kiwanda maeneo yale pia, kwani labda ndiyo sababu inayopelekea kiwanda cha Sikonge kishindwe kufanya kazi kwa haraka?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nachukua nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Jacqueline kwa kazi nzuri anayoifanya ya kufuatilia sekta hii ya asali katika Mkoa wa Tabora.

Mheshimiwa Naibu Spika, tutafuatilia, lakini taarifa za awali zilizonesha kuwa kulikuwa na changamoto za uendeshaji wa kiwanda kile cha awali cha Sikonge ambacho tulizindua mwaka 2023 chini ya Mheshimiwa Kakunda ambaye alifanya kazi kubwa sana kuvutia pale Sikonge kujengwa kiwanda hicho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutafuatilia tuone changamoto ni nini? Pamoja na hayo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba kama kweli tutajiridhisha kuwa kulingana na umbali huo aliousema kutoka Kiwele mpaka Kiwanda hiki cha Sikonge, na kama uzalishaji ni mkubwa na wa kutosha kuweza kuvutia wawekezaji katika Tarafa hii ya Kiwele, namhakikishia Mheshimiwa Jacqueline kwamba tutafanya hivyo kwa sababu tayari kuna wawekezaji wengi ambao wako tayari kujenga viwanda kupitia sekta binafsi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutafanya hivyo ili kurahisisha uchakataji wa asali katika tarafa hii ambayo Mheshimiwa Mbunge anaizungumzia, ahsante.