Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 1 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 15 2025-04-08

Name

Dr. Paulina Daniel Nahato

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza uhaba wa mabweni katika vyuo vikuu vya umma?

Name

Prof. Adolf Faustine Mkenda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rombo

Answer

WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya uhaba wa malazi ya wanafunzi katika vyuo vikuu vya umma nchini. Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inaendelea na ujenzi wa mabweni mapya 26 katika kampasi 12 za vyuo vikuu vya umma nchini. Mabweni haya yakikamilika yatakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 5,987 kwa wakati mmoja. Ujenzi wa majengo ya mabweni hayo unatarajiwa kukamilika mwaka 2026.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali inatoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza kwenye ujenzi wa hostel katika maeneo ya vyuo vikuu ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma ya malazi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.