Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Paulina Daniel Nahato

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza uhaba wa mabweni katika vyuo vikuu vya umma?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri, hasa pale aliposema kwamba sekta binafsi iwekeze. Hapo nimepapenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumwuliza maswali mawili ya nyongeza. Mwezi wa Tano, wanafunzi wa Form Six wanamaliza mitihani, na mojawapo ya ufaulu wa wanafunzi ni uhakikisho wa sehemu wanakolala. Je, tumejipanga vipi hao wanafunzi wakimaliza mitihani waweze kupata sehemu za kulala, wajue kabisa wanakwenda chuo fulani na wanapata mahali pa kulala? Swali la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Mloganzila ni eneo kubwa sana na ina hospitali. Kwa nini tunabanana pale Muhimbili? Eneo kubwa lile la Mloganzila lingetumika. Basi hao wawekezaji wapewe hilo eneo wajenge mabweni mengi sana ili wanafunzi wetu wapate mahali pa kukaa, ahsante sana.

Name

Prof. Adolf Faustine Mkenda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rombo

Answer

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Dkt. Nahato, kwamba naye ni mpiganiaji sana ya maslahi ya vyuo vikuu hapa nchini. Kwamba, tunahitaji kuwa na uhakika zaidi wa sehemu za kulala, kwa sasa hivi chuo ambacho tuna uhakika 100% wanafunzi wakienda wanaweza wakapata sehemu za kulala ni UDOM, Chuo Kikuu cha Dodoma. Vyuo vingine ni wastani wa 30% mpaka 50%.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza katika jibu la swali la awali, ni kwamba, Serikali sasa hivi inawekeza sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuongeza na kupanua wigo wa kampasi za kulala, na vilevile kuvutia hata kwenye utaratibu wa PPP, sekta binafsi kuja kuwekeza kwa ajili ya kuwa na hostel za wanafunzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili la nyongeza, Mloganzila ni pakubwa, ni kweli, na tayari napo ni sehemu ambapo tunajenga, tunafanya upanuzi kwa ajili ya kuongeza makazi ya wanafunzi. (Makofi)