Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 339 2025-05-19

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza:-

Je, lini Serikali itafanya ukarabati na kuongeza majengo ya Maabara katika Kituo cha Afya cha Mwika?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Mwika kilijengwa Mwaka 1905. Kituo hicho ni miongoni mwa vituo vya afya Kongwe 203 ambavyo Ofisi ya Rais TAMISEMI ilivifanyia tathmini kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu yake.

Mheshimiwa Spika, Serikali inakamilisha ukarabati wa hospitali 50 kongwe nchini na baada ye itafanya ukarabati wa vituo vya afya na zahanati kongwe kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya cha Mwika. Ahsante.