Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati na kuongeza majengo ya Maabara katika Kituo cha Afya cha Mwika?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ninaomba niulize maswali mawili ya nyongeza.  Swali la kwanza; nilipouliza swali kama hili kuhusu ukarabati wa Kituo hiki cha Mwika, Serikali iliniambia kwamba kiko kwenye mradi unaotekelezwa kwa ufadhili wa World Bank na kituo hiki kilikuwa namba 64 kwenye ile orodha. Ninaomba Waziri anihakikishie kama mradi huu umeanza kutekelezwa kimesha-move kwenda namba ngapi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kuna kituo cha afya cha mkakati ambacho tulipendekeza kule Vunjo kijengwe pale Kilwa Vunjo Kusini kwenye eneo la Koresa (ni kati ya vile vituo ambavyo vimeombewa shilingi milioni 250). Ninaomba Waziri atoe kauli kwamba; je, fedha hizo zimeshakwenda? (Makofi)
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei kwamba Kituo cha afya cha Mwika ni miongoni mwa vituo vya afya ambavyo vimewekwa kwenye mpango wa ukarabati kupitia Mfuko wa Benki ya Dunia (World Bank) na tayari tumeshakiainisha kwa ajili ya kupelekewa fedha za ukarabati. Hata hivyo, tumeanza na ukarabati wa hospitali za halmashauri, tunakwenda kujenga vituo vya afya kwenye kata za kimkakati ambazo hazina vituo vya afya lakini baadaye tutakwenda kukarabati vituo hivyo. 
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Kimei kwamba Kituo cha Afya cha Mwika kipo kwenye orodha ya World Bank na fedha zitapelekwa kwa ajili ya ukarabati na kimewekwa kwenye round ya pili kwenye Mfuko huo wa Dunia. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie yeye na wananchi wa Jimbo la Vunjo kwamba Kituo hiki Serikali hii sikivu ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hasan inatambua kwamba ni kikongwe na ni chakavu. Pia, nimhakikishie tu kwamba fedha zitakwenda kwa ajili ya ukarabati.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuhusiana na Kituo cha Afya cha Kilwa Vunjo. Mheshimiwa Kimei aliwasilisha Kata ya kimkakati na tayari Mheshimiwa Rais ameanza kutoa fedha katika majimbo 120 ya mwanzo. Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi wameanza kupokea fedha hizo katika kata za kimkakati na zoezi la kupeleka fedha hizo linaendelea. Kwa hiyo, nimakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika Kata hiyo pia ya Kilwa-Vunjo, fedha zitakwenda wakati wowote ili kituo hicho kiweze kujengwa.
							
 
											Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati na kuongeza majengo ya Maabara katika Kituo cha Afya cha Mwika?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itapeleka pesa katika Kituo cha Afya Kata ya Udekwa kwa sababu wananchi wanatembea umbali mrefu sana kufuata matibabu mpaka Ilula zaidi ya kilometa 50? Ahsante sana.
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, moja ya vigezo vya kupeleka vituo vya afya katika kata za kimkakati ni umbali mkubwa wa kituo cha afya au kata ambayo inahitaji kituo hicho kutoka Kituo cha afya kilicho jirani zaidi.
Mheshimiwa Spika, ninaomba tu nichukue hoja ya Mheshimiwa Mbunge Dkt. Ritta Kabati kuhusiana na Kituo cha Afya cha Kata ya Udekwa na tutakwenda kufanya tathmini ikiwa kinakidhi vigezo vya idadi ya wananchi na umbali wa kilometa 50, basi tutaona namna ya kuweka kwenye mpango mkakati kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo hicho cha afya.  Ahsante sana.
							
 
											Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati na kuongeza majengo ya Maabara katika Kituo cha Afya cha Mwika?
Supplementary Question 3
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ninaishukuru Serikali kwa kutoa shilingi milioni 250 tayari sisi tumeshazipokea kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Busolwa. Swali; ni lini sasa Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kujenga nyuma ama jengo la mama na mtoto kwenye Kituo cha Afya Nyijundu pamoja na Kafita? Ahsante. (Makofi)
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninamshukuru Mheshimiwa Amar kwamba jimbo lake tayari wameshapokea shilingi milioni 250 ambazo zilikuwa ni ahadi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa majimbo yote 214. Hii ni habari njema kwa Waheshimiwa Wabunge wote wa majimbo haya ambao wameanza kupata hizo fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivyo. 
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niwahakikishie kwanza Waheshimiwa Wabunge, kwa kuwa jambo hili limekuwa likifuatiliwa mara kwa mara kwamba Serikali imeanza kupeleka fedha hizo tuwe na Subira, lakini tuendelee kuwasiliana na wakurugenzi wa halmashauri kuona kama fedha zimeingia kwa ajili ya kuanza utekelezaji mapema iwezekanavyo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu vituo vya afya ambavyo Mheshimiwa Mbunge amevitaja, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ikiwa vituo hivyo vinakidhi vigezo vya kata za kimkakati, Serikali kwa awamu itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga vituo hivyo. Kwa hivyo ninaomba awasilishe kata hizo na sisi tutazifanyia kazi kuona kama zinakidhi vigezo ili kazi za ujenzi zianze kutekelezwa.  Ahsante.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved