Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 54 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 691 2025-06-26

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: -

Je, lini Zahanati za Molemlimani, Muungano, Urafiki, Isanjandugu, Iyombakuzova na Kapumpa zitakamilika?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kujenga vituo vya kutolea huduma na kuvisajili ili vianze kutoa huduma za afya. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 jumla ya zahanati 1,158 zimejengwa na kusajiliwa na zinatoa huduma.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge itatenga shilingi milioni 250 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya Zahanati za Muungano, Urafiki, Isanjandugu, Iyombakuzova, Kapumpa na Molemlimani. Ahsante. (Makofi)