Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 340 2025-05-19

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mwasayi ambacho kimepelekewa vifaatiba lakini hakina majengo ya kutosha?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Mwasayi kilianza kutoa huduma katika ngazi ya zahanati mwaka 1962 na kupandishwa hadhi mwaka 1977 na kuanza kutoa huduma ngazi ya kituo cha afya. Aidha, majengo ya kituo hiki ni machache na chakavu.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi na jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Mwasayi.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga na kupeleka fedha kwenye halmashauri zote nchini kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu iliyosalia ili vituo vya afya viweze kutoa huduma stahiki.