Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mwasayi ambacho kimepelekewa vifaatiba lakini hakina majengo ya kutosha?

Supplementary Question 1

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Spika, ninaipongeza Serikali na kuishukuru kwa kupeleka fedha hizo shilingi milioni 250 na asubuhi hii nimehakikisha kupitia Mkurugenzi wangu kwamba fedha hiyo imekwishafika. Kwa vile, wananchi wa Kata ya Zanzui na Kata ya Kadoto pia wameshaanza ujenzi wa vituo viwili vya afya kwenye hizo kata; je, Serikali iko tayari kuunga mkono juhudi za wananchi hao? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita siku zote imekuwa tayari kuwaunga mkono wananchi katika ujenzi wa vituo vya huduma ya afya, kama ambavyo tayari imeshapeleka shilingi milioni 250 kwenye Kituo cha Afya cha Mwasayi. Nimhakikishie, katika Kata hizo za Zanzui na hiyo nyingine ambayo ameitaja tutahakikisha pia tunaanza kutenga fedha kwenye bajeti zetu kwa ajili ya kuchangia nguvu za wananchi katika ujenzi wa vituo hivyo vya afya kwa awamu. Ahsante sana.

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mwasayi ambacho kimepelekewa vifaatiba lakini hakina majengo ya kutosha?

Supplementary Question 2

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Makorongo kilianza kutumika miaka 10 iliyopita kikiwa hakina majengo ya OPD na maabara. Ninataka kujua ni lini Serikali itatoa fedha ili kukamilisha ujenzi huo? Ahsante sana.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kwamba vipo vituo vya afya ambavyo vimeanza kutoa huduma, lakini vina upungufu wa majengo muhimu kwa ajili ya huduma hizo kikiwepo kituo cha afya ambacho Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Chemba amekitaja.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mbunge kwamba, tayari Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI tulishaainisha vituo vya afya vyenye majengo pungufu na vituo vya afya chakavu na kongwe 203 na tayari tumeanza kuandaa bajeti kwa awamu kwa ajili ya ukarabati wa vituo hivyo vya afya ili viweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie pia Mheshimiwa Mbunge, majengo hayo ya maabara, wodi ya wanawake, wanaume na majengo mengine yatakwenda kujengwa kwenye kituo hicho cha afya. Ahsante.