Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 341 2025-05-19

Name

Rehema Juma Migilla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga sekondari nyingine katika Kata ya Kanindo kwa kuwa Shule ya Sekondari Kanindo ina wanafunzi wengi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Shule ya Sekondari Kanindo ina wanafunzi 648 wa kidato cha kwanza hadi kidato cha nne wakijumuisha wavulana 255 na wasichana 393.

Mheshimiwa Spika, shule hiyo ina vyumba vya madarasa 19 ambavyo vinatosheleza mahitaji kwa wanafunzi waliopo. Aidha, shule ina hosteli inayohudumia wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali kikiwemo Kijiji cha Mbeta. Vilevile, baadhi ya wanafunzi wamehamishiwa shule mpya ya Ikonongo kwa lengo la kuwapunguzia mwendo mrefu wa kutembea.