Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Union Affairs Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 342 2025-05-19

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza kazi ya kurejesha Mto Kondoa katika njia yake ya asili?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) imefanya upembuzi yakinifu kwa lengo la kubaini chanzo cha kuhama kwa Mto Kondoa. Miongoni mwa sababu zilizobainika ni pamoja na uwepo wa shughuli za kibinadamu zisizo endelevu, kama vile ufugaji, kilimo, ujenzi na uchimbaji wa madini ndani ya meta 60 zinazosababisha kuongezeka kwa upana wa kingo za mto na kupungua kwa kina kutokana na kujaa kwa udongo ndani ya wa mto. Hali hii imesababisha wakati wa mvua maji kuacha njia yake ya asili na kuelekea kwenye maeneo mengine na kuleta uharibifu wa mashamba na mmomonyoko wa udongo.

Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na athari hizo, Serikali inaendelea kutoa elimu kwa umma, kuhamasisha jamii kuacha kufanya shughuli zisizo endelevu ndani ya meta 60 za mto husika, ili kupunguza tatizo la kuhama kwa mto huo mara kwa mara. Aidha, ninaomba kutoa rai kwa wananchi kuendelea kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191, wanapofanya shughuli za kibinadamu ili kukabiliana na uharibifu wa Mazingira.

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. (Makofi)