Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo 343 2025-05-19

Name

Seif Khamis Said Gulamali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manonga

Primary Question

MHE. AZIZA S. ALLY K.n.y. MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza:-

Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa Viwanja vya Michezo Sekondari ya Ziba, Manonga?

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Answer

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA, NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inayo nia ya dhati ya kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo katika shule zote nchini kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha. Michezo kwa sasa huzalisha ajira kwa vijana, hulitangaza Taifa Kimataifa pamoja na kuliletea heshima. Hivyo, ninakiri uwekezaji katika viwanja vya michezo shuleni ni muhimu.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Wizara haina bajeti ya kuwezesha ujenzi wa viwanja katika Shule ya Sekondari Ziba, iliyopo Manonga. Wizara ipo tayari kutuma wataalam katika shule hiyo, kwa ajili ya kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu ujenzi wa miundombinu ya viwanja. Aidha, Wizara inaushauri Uongozi wa Shule ya Sekondari Ziba kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Tabora ambao ni wadau wakubwa wa Wizara katika Sekta ya Michezo, ili kufanikisha ukarabati wa viwanja vya michezo shuleni, ikiwemo Shule ya Sekondari ya Ziba. (Makofi)