Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 344 2025-05-19

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Kiwanda cha Ngara Arab Globe cha kuchakata Kahawa ghafi, ili kuongeza thamani ya Zao la Kahawa?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha kuchakata kahawa cha Ngara Arab Globe International Limited ni kiwanda cha wawekezaji (Sekta Binafsi) kinachomilikiwa na Watanzania na Wanyarwanda. Hata hivyo, kiwanda hiki kwa sasa hakifanyi kazi kutokana na changamoto ya Wawekezaji kushindwa kuhimili ushindani wa kibiashara.

Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto hiyo, Serikali imechukua hatua ya kukutana na wawekezaji wa kiwanda na kuwashauri kutafuta wabia wenye nia na uwezo wa kuwekeza katika Sekta ya Kahawa.