Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Kiwanda cha Ngara Arab Globe cha kuchakata Kahawa ghafi, ili kuongeza thamani ya Zao la Kahawa?

Supplementary Question 1

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu ya Serikali. Kahawa ya Tanzania imekuwa ikiuzwa nje, ikiwa bado ni ghafi bado haijawa processed, sasa ninataka kuuliza; je, Serikali ina mpango gani wakuwavutia au kuwakaribisha wawekezaji waje kuwekeza kwenye viwanda ili kahawa ya Tanzania iweze kupanda bei?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer


NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nipende kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bilakwate, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kwamba Serikali inafanya juhudi mbalimbali za kuwafanya wawekezaji wawe karibu sana na nchi yetu, kwa maana ya kufanya maboresho mbalimbali. Ndiyo maana katika kiwanda hiki tumekaa na wawekezaji waliowekeza ambao kimsingi uwezo wao ni mdogo na kuwashawishi waweze kuingia ubia na watu wenye uwezo ili kuhakikisha kwamba kahawa yetu inapata ufanisi wa kutosha katika maboresho ya hatua za awali kabla ya kuingia kwenye soko.