Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Works, Transport and Communication Wizara ya Uchukuzi 345 2025-05-19

Name

Maulid Saleh Ali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Welezo

Primary Question

MHE. MAULID SALEH ALI aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga uzio wa umeme kwenye Reli ya SGR kutoka Ngerengere hadi Dodoma?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Shirika la Reli (TRC) ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa ujenzi wa uzio katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kipande cha Morogoro hadi Dodoma. Hivi sasa, ujenzi wa uzio huo umefikia 95.12%. TRC inaendelea kumsimamia mkandarasi ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kwa wakati.