Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maulid Saleh Ali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Welezo

Primary Question

MHE. MAULID SALEH ALI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga uzio wa umeme kwenye Reli ya SGR kutoka Ngerengere hadi Dodoma?

Supplementary Question 1

MHE. MAULID SALEH ALI: Mheshimiwa Spika, nishukuru kwa majibu mazuri ya Serikali; nitauliza swali moja. Kutokana kwa kuhamasika kwa wananchi kutumia usafiri wa treni ya SGR. Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza route zake kutoka Dodoma – Dar es Salaam?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninamshukuru Mheshimiwa Maulid Saleh Ali, kwa swali lake la nyongeza. Ninakubaliana naye kwamba tangu usafiri wa treni ya SGR ulipoanzishwa mwamko umekuwa ni mkubwa sana kwa Watanzania, wamefurahia huduma hii na mahitaji yameongezeka zaidi. Kutokana na hali hiyo tayari hivi ninavyozungumza timu ya wataalam imeshaanza kufanya kazi ili kuchambua na kutazama mahitaji halisi ili hatimaye sasa tuweze kufikiria tuanzishe route pengine ziwe lini. Kwa sababu ukiangalia weekend mahitaji yanakuwa makubwa zaidi kuliko katikati ya wiki; kwa hiyo wataalam wanafanya kazi yao.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Maulid na Waheshimiwa Wabunge wengi ambao kimsingi wamekuwa wakifuatilia jambo hili, timu hiyo itakapokamilika tayari Mheshimiwa Waziri wetu, Mheshimiwa Mbarawa ameelekeza kwamba kazi hiyo ianze mara moja, route hizo ziongezwe. Jambo jema na zuri ni kwamba tayari Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alikwishatupatia fedha na vitendea kazi vipo vya kutosha; kwa hiyo tunaamini kwamba kazi hiyo inakwenda vizuri zaidi. (Makofi)

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. MAULID SALEH ALI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga uzio wa umeme kwenye Reli ya SGR kutoka Ngerengere hadi Dodoma?

Supplementary Question 2

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa reli ya SGR kutoka Jijini Dar es Salaam, kupitia Lindi na Mtwara hadi Mbamba Bay? (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, samahani, kutoka Dar es Salaam?

SPIKA: Kutoka Dar es Salaam, kupitia Mtwara mpaka Mbamba Bay.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, nimshukuru Mheshimiwa Ndulane kwa swali lake zuri. Kwa sasa Serikali haijaanza upembuzi yakinifu wala usanifu wa kina kuhusiana na reli kutoka Dar es Salaam kwenda Lindi. Hata hivyo, kwa kutambua umuhimu mkubwa wa reli ya kusini, yaani kutoka Mtwara Port kwenda mpaka Mbamba Bay kupitia matawi ya Liganga na Mchuchuma tayari tumeshakamilisha study.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi Serikali ipo kwenye hatua ya utafutaji wa fedha ili kuweza kuunganisha kipande hicho kiweze kujengwa kwa njia ya SGR; na kutokana na umuhimu mkubwa wa makaa ya mawe ambayo tuna zaidi ya makaa ya mawe zaidi ya metric tons milioni 428, tuna chuma cha kutosha, lakini pia ni kutekeleza maoni ya waasisi wa nchi zetu hizi za Malawi, Tanzania pamoja na Msumbiji katika kuhakikisha kwamba tunaziunganisha kupitia Ziwa Nyasa na Bahari ya Hindi.

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAULID SALEH ALI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga uzio wa umeme kwenye Reli ya SGR kutoka Ngerengere hadi Dodoma?

Supplementary Question 3

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itaanza ile ahadi yake ya kutengeneza reli ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro? Ahsante sana.

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa swali lake Mheshimiwa Shally Raymond. Ni kweli kabisa kwamba Serikali inao mpango wa kujenga reli ya kisasa SGR inayounganisha Tanga kwenda mpaka Arusha kuunganisha mpaka Musoma na hii ni kutokana na uwepo wa madini ya kutosha ya nickel kule Dutwa, madini ya magadisoda kule Engaruka pamoja na kule Minjingu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii pia kueleza pia vizuri. Reli hii ya kisasa ni gharama kubwa sana kuijenga, kwa hiyo unapoamua kufanya maamuzi ya kujenga lazima uwe na uhakika na mzigo uliopo. Kipande hiki tayari tumeshajiridhisha mzigo upo wa kutosha. Kwa sasa tumeshakamilisha study tupo kwenye hatua za utafutaji wa fedha ili tukikamilisha tuweze kuanza kujenga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunajenga kilometa 2,300 kwa sasa hivi. Tuna kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza, tuna kutoka Tabora mpaka Kigoma na tumeanza kutoka Uvinza mpaka Burundi. Hivyo sio rahisi tukafanya mambo yote kwa wakati mmoja, hizi kilometa 2,300 hakuna nchi Barani Afrika imewahi hata kufikiria na hivyo inaifanya nchi yetu na kumfanya Dkt. Samia, kuwa ndiye Rais, kinara wa reli ya kisasa Barani Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, reli hii ya kisasa anayoijenga Dkt. Samia, inamfanya kuwa ndiye Rais, kinara wa ujenzi wa reli ya kisasa Barani Afrika na kumfanya kuwa wa tano duniani. Niwaombe Waheshimiwa Wabunge, tuvumilie amalize kazi hii ambayo ameshaianza ili baadaye tuweze kuanza na sehemu hizo zingine ambazo kimsingi wamekuwa wakizihitaji.