Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 346 2025-05-19

Name

Tamima Haji Abass

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza:-

Je, upi mpango wa Serikali kuimarisha mawasiliano ya simu kwenye vijiji vyenye changamoto ya huduma hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Mwaka wa Fedha 2021/2022 ilitekeleza mradi wa kimkakati wa kufikisha mawasiliano katika Shehia 38 zilizokua na changamoto ya mawasiliano, ambapo jumla ya minara 42 ilijengwa kwa kushirikiana na mtoa huduma Honora (YAS). Kati ya minara hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja ulinufaika kwa kujengewa minara 12. Mradi huu ulikamilika kikamilifu na kwasasa wananchi wananufaika na huduma za mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge, ameuliza swali kuhusu jitihada za Serikali katika kutatua changamoto ya mawasiliano ya simu katika vijiji vya Mkoa wa Kaskazini Unguja, inaashiria kuwa bado kuna changamoto. Wizara kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itafanya tathmini kwenye mkoa husika ili kubaini mahitaji halisi ya mawasiliano. Endapo ikibainika kuwepo kwa tatizo la mawasiliano katika mkoa huo, utaingizwa katika zabuni ya miradi itakayotekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2025/2026. (Makofi)