Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tamima Haji Abass

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali kuimarisha mawasiliano ya simu kwenye vijiji vyenye changamoto ya huduma hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja?

Supplementary Question 1

MHE. TAMIMA HAJI ABASS: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nitakuwa na swali moja la nyongeza. Kama alivyosema kama bado kuna changamoto, ni kweli. Je, yupo tayari tuambatane kwenda Kijiji cha Tazari kwenda kuona hali halisi na kutufanyia namna ya uharaka wa mawasiliano hayo? Ahsante sana.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Tamima. Kuhusiana na suala la utayari, kama tulivyoongea mara nyingi kuhusiana na hili eneo la Tazari Jimbo la Nungwi, tayari nimeagiza wataalam saa saba watamtafuta, wataongea kwa kina ili kupanga namna njema ya kwenda kufanya ziara. Ahsante.

Name

Khalifa Mohammed Issa

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Mtambwe

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali kuimarisha mawasiliano ya simu kwenye vijiji vyenye changamoto ya huduma hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja?

Supplementary Question 2

MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza niruhusu nimpongeze Naibu Waziri kwa kutekeleza ahadi yake hapa Bungeni ya kuja Mtambwe, Kijiji cha Kidundo, na alikuja akakutana na wananchi. Je, ni lini utekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Naibu Waziri pale ama kujengewa minara, mradi wananchi wapate mawasiliano ya simu?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, nipokee pongezi; ule mradi tayari upo kwenye mpango mzuri, kadri fedha tunavyozipata na yenyewe ipo kwenye mgawo, wanakuja kutekeleza. Nilijionea ile kadhia, kwa hiyo wananchi wale wanaletewa mawasiliano ya uhakika. Ahsante.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali kuimarisha mawasiliano ya simu kwenye vijiji vyenye changamoto ya huduma hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja?

Supplementary Question 3

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Hai bado kuna vijiji mbalimbali havina mtandao na wananchi wanapata tabu. Kwa mfano, Kata ya Kia, Mtakuja na Sanya Station. Pia Kata ya Masama Magharibi, Masama Kati, Masama Mashariki na Machame Kaskazini Kijiji cha Uduru Mwana maeneo haya mtandao hakuna. Serikali ina mpango gani...

SPIKA: Mheshimiwa Saashisha, hilo bado ni swali la nyongeza, vijiji vyote hivi? Haya uliza swali lako.

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha vijiji hivi vinapata mawasiliano ya hakika?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba maeneo yote tunayafikia na wananchi wa maeneo hayo yote aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge, tunawapa mawasiliano ya uhakika.

Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu, kadri tunavyopata fedha, hasa mwaka ujao wa fedha, tutahakikisha wataalam wanakuja wanafanya tathmini ya ukubwa wa changamoto; na nimhakikishie kuwa tutajenga minara na kuleta mawasiliano ya uhakika. Ahsante.

Name

Robert Chacha Maboto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda Mjini

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali kuimarisha mawasiliano ya simu kwenye vijiji vyenye changamoto ya huduma hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja?

Supplementary Question 4

MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Spika, Jimbo la Bunda Mjini, Kata ya Mcharo, Mtaa wa Kiharagweta mawasiliano ya simu yapo chini sana. Je, Serikali ina mpango gani katika kuhakikisha kwamba inaboresha mawasiliano katika maeneo hayo? Ahsante.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maboto. Hapa kati ya mji kama mawasiliano yapo hafifu tutatuma wataalam wetu kuja kupima, kufanya tathmini ya changamoto. Hapa ninaona ni suala tu la uboreshaji na ku-upgrade. Kama ni 2G tuweke angalau 3G, 4G ili mawasiliano yaweze kupatikana. Ahsante.

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali kuimarisha mawasiliano ya simu kwenye vijiji vyenye changamoto ya huduma hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja?

Supplementary Question 5

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, Serikali ilikuwa na mpango wa kupeleka mawasiliano katika Kata ya Kihanga na imefanikiwa kupeleka katika Kijiji cha Igangidung’u lakini bado Kijiji cha Makombe. Je, ni lini sasa Serikali itatupelekea mawasiliano huko Makombe? Ahsante sana.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge. Kijiji cha Makombe nacho tutakiweka katika mpango kazi wa mwaka ujao wa fedha, kadri fedha zitakavyopatikana. Ahsante.