Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 348 2025-05-19

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Daraja la Mto Malagarasi katika Tarafa ya Ilagala – Uvinza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Daraja la Malagarasi ya Chini lenye urefu wa mita 200 katika Barabara ya Simbo – Ilagala hadi Kalya yenye urefu wa kilometa 234 imekamilika. Kwa sasa, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.