Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Daraja la Mto Malagarasi katika Tarafa ya Ilagala – Uvinza?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwanza nimshukuru kwa majibu yake ya kujirudiarudia, hii ni mara ya nne nikiwa ninauliza swali hili. Swali la kwanza, ninaomba kujua utekelezaji huu utaanza lini?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; daraja hili lina manufaa ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Kigoma. Je, hawaoni kuwa kuna haja ya kufanya haraka?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Josephine Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum, Kigoma kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, atakubaliana nami hapa hapakuwa na Daraja, tulikuwa tunavusha kwa vivuko, tumeshasanifu tumeshakamilisha. Pia nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge daraja hili litagharimu shilingi bilioni 24 na bahati nzuri ni kati ya madaraja ambayo yanaenda kutekelezwa kwa fedha ya World Bank na tunavyoongea sasa hivi World Bank wamesharidhia hizo hela zipatikane ili tuweze kujenga na kuacha na kivuko cha kwenda Kalya ambacho tunajua changamoto zilizokuwepo. Mheshimiwa Dkt. Samia, ametafuta fedha na tunakwenda kuanzisha hilo daraja muda si mrefu. Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Daraja la Mto Malagarasi katika Tarafa ya Ilagala – Uvinza?

Supplementary Question 2

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tija ya Bandari ya Ndumbi inategemea sana kukamilika kwa Barabara itakayojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Rwanda hadi Ndumbi, barabara hiyo imeshasainiwa. Ni lini fedha itatolewa ili mkandarasi aanze kazi mara moja? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli tunatambua umuhimu wa hiyo barabara na tayari tumeshapata mkandarasi tumeshasaini, tunachosubiri ni kumlipa huyo mkandarasi ili kazi ianze. Kwa kweli ameshaleta maombi ya malipo ya awali na Serikali tunatafuta fedha tumlipe ili kazi hiyo ianze ya kujenga hiyo barabara kwa kiwango cha lami kutoka Rwanda hadi Ndumbi. Ahsante.

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Daraja la Mto Malagarasi katika Tarafa ya Ilagala – Uvinza?

Supplementary Question 3

MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Chapwa - Chiwezi - Chindi - Msangano ilikuwa ni ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, alipotutembelea mwaka 2020. Ninataka kufahamu barabara hii imefikia hatua gani hasa katika ujenzi wa daraja katika mto uliopo pale Chindi? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Tutawasiliana na wenzetu wa TARURA kwa sababu hii barabara bado inahudumiwa na wenzetu wa TARURA tujue wapi Serikali imefikia katika kuitekeleza hii ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Ahsante.