Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 349 2025-05-19

Name

Godwin Emmanuel Kunambi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlimba

Primary Question

MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:-

Je, lini Mkandarasi atapatikana na kuanza ujenzi wa Barabara ya Morogoro hadi Njombe Border kutoka Ifakara hadi Chita?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza ujenzi wa Barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Madeke hadi Kibena yenye urefu wa kilometa 346.43 kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ambapo kwa sehemu ya Kwanza ya Ifakara – Mbingu (kilometa 62.5) ujenzi unaendelea na Mkandarasi wa sehemu ya Pili ya Mbingu – Chita (kilometa 37.5) ameanza maandalizi ya ujenzi.

Mheshimiwa Spika, kwa sehemu ya Kibena – Kidegembye (kilometa 42) taratibu za ununuzi ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami zipo katika hatua za mwisho. Aidha, kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina unaendelea kwa sehemu ya Kihansi – Mlimba hadi Madeke yenye urefu wa kilometa 95.26. Ahsante. (Makofi)