Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Godwin Emmanuel Kunambi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mlimba
Primary Question
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:- Je, lini Mkandarasi atapatikana na kuanza ujenzi wa Barabara ya Morogoro hadi Njombe Border kutoka Ifakara hadi Chita?
Supplementary Question 1
MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Spika, kwanza, nikushukuru wewe binafsi, ulipata fursa ya kupita kwenye barabara hii wakati umetembelea jimboni kwangu, Mungu akubariki sana baada tu ya wewe kutembelea jimboni kwangu Serikali ililipa part payment ya mkandarasi wa kwanza. Ninaomba niulize maswali yangu mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kipande hiki cha kutoka Ifakara hapa Mbingu kilometa 62.5, habari ya kwamba mkandarasi kazi inaendelea, sasa yapata miaka miwili mkandarasi yupo site tangu alipwe shilingi 5,000,000,000, bado nne tu anasema akilipwa aanze kazi.  Ninaomba majibu ya uhakika ya Serikali, ni lini Serikali itamalizia hizo shilingi 4,000,000,000 ili mkandarasi huyu afanye kazi hiyo? Kwa sababu yupo site miaka miwili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kipande cha kutoka Mbingu - Chita kilometa 37.5. Je, naye huyu mkandarasi atalipwa lini? Ahsante. (Makofi)
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
								NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:- 
Mheshimiwa Spika, kwanza, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba siku zote majibu ya Serikali ni ya uhakika na hata haya nitakayotoa ama niliyoyatoa ni ya uhakika. Kipande cha Ifakara – Mbingu kama alivyosema tumeshamlipa sehemu ya malipo mkandarasi ambaye yupo site na atakubaliana nami kwamba kwa sasa kwa kweli eneo hilo mvua inanyesha nyingi na ni vigumu sana kwa mkandarasi kufanya kazi kubwa hasa zile tunazoita za earth work. 
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge hali itakapotengamaa mkandarasi yupo site na ataendelea kufanya kazi. Kwa sasa nadhani atakubaliana nami anaendelea kuziba mashimo au kurudishia mawasiliano yanapokuwa yamekatika.
Mheshimiwa Spika, kuhusu kipande cha pili, Mbingu - Chita kama alivyosema tayari mkandarasi tumeshampata na tumhakikishie kwamba tayari Wizara ya Fedha inafanya taratibu za kumlipa malipo ya awali ili naye aanze hiyo kazi. Ahsante.
							
 
											Name
Jafari Chege Wambura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rorya
Primary Question
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:- Je, lini Mkandarasi atapatikana na kuanza ujenzi wa Barabara ya Morogoro hadi Njombe Border kutoka Ifakara hadi Chita?
Supplementary Question 2
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi na niishukuru Serikali kwa kuridhia kutangaza Barabara ya Utegi - Shirati kwenda Kilongwe kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami. Pamoja na hayo Mheshimiwa Naibu Waziri, Barabara ya Kuruya – Kumoge- Kinesi ni lini upembuzi yakinifu ya barabara hii utakamilika kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami?
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nimhakikishie Mheshimiwa Chege, Mbunge wa Rorya kwamba barabara aliyoitaja kwa mujibu wa taratibu za usanifu hakuna kitakachokwamisha kwa sababu haitegemei mvua ama hali ya hewa. Kwa mujibu wa mkataba ulivyo, tutahakikisha kwamba usanifu unakamilika kwa muda kama tulivyopanga kwenye mkataba. Ahsante.
 
											Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:- Je, lini Mkandarasi atapatikana na kuanza ujenzi wa Barabara ya Morogoro hadi Njombe Border kutoka Ifakara hadi Chita?
Supplementary Question 3
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Ruanda – Iyula – Idiwili - Nyimbili hadi Vwawa ni lini wakandarasi wanawake watapatikana ili kuanza ujenzi? Ahsante sana. (Makofi)
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
								NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwanza, nimshukuru Mheshimiwa Mbunge, kwa swali hili zuri na nilieleze Bunge kwamba katika hii awamu moja ya mambo ambayo tumeyafanya kwa barabara aliyouliza, ni Mheshimiwa Rais kuelekeza kwamba wakandarasi wanawake waweze kupewa kazi na hii barabara imegawanywa, ina kilomita 20 wale wakandarasi wote wanawake ambao watafanya wamepewa kilometa tano tano ambayo ndiyo hiyo barabara anayoongelea. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tunavyoongelea sasa hivi tupo kwenye hatua za manunuzi ili wakandarasi hao waanze kazi hiyo ya kujenga hiyo barabara ya kilometa 20. Kilometa moja imeshajengwa, lakini hizo kilometa 20 muda si mrefu zinaanza kujengwa na tuna hakika zitaanza kujengwa kabla ya mwaka huu wa fedha 2024/2025 kwisha. Ahsante. (Makofi)
							
 
											Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:- Je, lini Mkandarasi atapatikana na kuanza ujenzi wa Barabara ya Morogoro hadi Njombe Border kutoka Ifakara hadi Chita?
Supplementary Question 4
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Makete - Mbeya mvua inanyesha miezi nane katika mwaka mkandarasi hajalipwa hadi sasa hivi. Ni ipi kauli ya Serikali malipo kwa mkandarasi huyu, ili afanye kazi kwa uhakika na kwa wakati? (Makofi)
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
								NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge ni kweli ni eneo ambalo lina mvua muda wote ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara zote ambazo wakandarasi wapo site, kama Wizara tumeshawasilisha maombi kwa maana ya mahitaji ya fedha ikiwemo hiyo barabara yake na tuna uhakika lazima tumlipe mapema ili hali ya hewa inavyokaa vizuri wakandarasi hao waanze kufanya kazi. Ahsante. (Makofi)
							
 
											Name
Mrisho Mashaka Gambo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arusha Mjini
Primary Question
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:- Je, lini Mkandarasi atapatikana na kuanza ujenzi wa Barabara ya Morogoro hadi Njombe Border kutoka Ifakara hadi Chita?
Supplementary Question 5
MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Barabara ya Arusha – Kibaya - Kongwa ambayo Arusha inategemea kujengewa kilometa 70. Je, ni lini mkandarasi atakwenda site maana mkataba ulishasainiwa tayari?
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
								NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara hii ilikuwa ndio moja ya zile barabara ndefu za EPC+F na Serikali iliamua ianze kujenga kutokea Arusha ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba zile barabara ambazo zitatumika AFCON ziwe ni sehemu ya hizo barabara.
Mheshimiwa Spika, tayari tumeshasaini mkataba na mkandarasi na wakandarasi hao wapo wanapitia kwa sababu ilikuwa ni barabara ndefu kuzifupisha na kuziweka katika zile kilometa 70 ambazo zitajengwa na muda si mrefu tunategemea kwamba tutawalipa malipo ya awali ili waweze kuanza kazi. Ahsante.