Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 27 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 350 2025-05-19

Name

Bonnah Ladislaus Kamoli

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Segerea

Primary Question

MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza:-

Je, namna gani Serikali inatekeleza takwa la Sera la ushirikishwaji wa Wazee katika shughuli za uzalishaji mali?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Sera ya Taifa ya Wazee imetambua umuhimu wa wazee kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kuinua kipato chao. Hivyo, Serikali kwa kushirikiana na wadau imeanzisha vikundi 395 vya uzalishaji mali vya wazee ambapo jumla ya wazee 10,926 (Me 5,333 na Ke 5,593) walinufaika na miradi mbalimbali ikiwemo ya kuwezeshwa kujihusisha na shughuli ndogo ndogo za kilimo cha mboga mboga, kuwa na vitalu vya miche ya matunda, ufugaji wa nyuki, mbuzi, ng’ombe na kuku.

Mheshimiwa Spika, niendelee kutoa wito kwa wazee kutumia mazingira yao kufanya shughuli ndogondogo ambazo zinasaidia kuimarisha afya ya mwili na akili. Aidha, ninasisitiza jamii kuendelea kuunga mkono juhudi na shughuli zinazofanywa na wazee katika jamii zetu ili kuimarisha ustawi wao. Ahsante.