Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Bonnah Ladislaus Kamoli
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Segerea
Primary Question
MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza:- Je, namna gani Serikali inatekeleza takwa la Sera la ushirikishwaji wa Wazee katika shughuli za uzalishaji mali?
Supplementary Question 1
MHE. BONNAH L. KAMOLI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa Serikali kwa kutoa majibu mazuri, lakini ninataka nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri, maswali mawili.  Swali la kwanza; programu ambazo zinafanyika zinaonekana kwamba zinafanyika kwa wazee waliopo Kijijini. Je, Serikali ina mpango gani na wazee ambao wanaishi mjini hasa Wazee wa Jimbo la Segerea?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kama tunavyojua kwenye programu nyingine ambazo zinaendelea kwa vijana pamoja na wanawake ambao wanapata 10%. Je, kwa nini, Serikali isianzishe programu ya kuwasaidia wazee ambao kama wanaopata vijana, wanawake na walemavu? (Makofi)
 
											Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante. Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, inajali sana wazee na inatoa fursa kwa wazee wote haina ubaguzi. Niwaombe tu wazee wakiwemo na Wazee wa Segerea kutumia fursa hizi kuhakikisha wanaendelea kupata maisha yao na uwezeshaji wa kiuchumi katika familia zao na kupata faraja katika maisha yao.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wazee na kupata fursa mbalimbali. Vilevile, sasa hivi kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii na kushirikiana na Wizara ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI, tunayo mikopo midogo midogo ambayo inawawezesha wananchi pamoja na wazee imechanganya watu wote kutumia fursa hizi waonane na Maafisa Maendeleo katika halmashauri zao ili kupata vitambulisho na kuchukua mikopo hiyo katika Benki za NMB ambayo tulishafunga nayo mikataba. Ahsante. (Makofi)
							
 
											Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza:- Je, namna gani Serikali inatekeleza takwa la Sera la ushirikishwaji wa Wazee katika shughuli za uzalishaji mali?
Supplementary Question 2
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itaweka mpango wezeshi kwa wazee katika Mkoa wa Mtwara ili kuwafanya wafanye shughuli ndogo ndogo za uzalishaji mali? Ahsante. (Makofi)
 
											Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wazee na nimwombe Mheshimiwa Mbunge afike katika Ofisi ya Halmashauri Kuu ya Mtwara waonane na Maafisa Maendeleo ili wazee hao wapate elimu na waweze kujiwezesha kiuchumi na kupata fursa na maisha ya kujiendeleza ili waone umuhimu wa Serikali yao ya Awamu ya Sita. Ahsante. (Makofi)
 
											Name
Vedastus Mathayo Manyinyi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Musoma Mjini
Primary Question
MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza:- Je, namna gani Serikali inatekeleza takwa la Sera la ushirikishwaji wa Wazee katika shughuli za uzalishaji mali?
Supplementary Question 3
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa zile fedha za uwezeshaji kwa ajili ya akinamama pamoja na vijana na watu wenye ulemavu zinatoka kwenye Halmashauri zetu. Ni kwa nini, sasa Serikali isianze kutenga fedha kutoka kwenye Bajeti Kuu ya Serikali kwa ajili ya kuongeza nguvu ili yale makundi yaweze kupata fedha za kutosha katika biashara zao?
 
											Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema Serikali inaendelea kutoa fursa mbalimbali kwa ajili ya kuwapa mikopo midogo midogo wafanyabiashara ndogo ndogo wakiwemo wazee. 
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema waende katika Halmashauri wakutane na Maafisa Maendeleo kuwapa elimu ili waweze kupata vitambulisho hivyo ili waweze kujiendesha na mifuko hiyo midogo midogo na biashara zao ziweze kukuwa. Ahsante.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved