Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 106 2025-04-22

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:-

Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa wodi ya upasuaji ya wanawake na jengo la kuhifadhia maiti Hospitali ya Wilaya ya Karatu?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imetenga shilingi milioni 800 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya upasuaji ya wanawake, jengo la kuhifadhia maiti pamoja na njia za kutembelea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Karatu. Ahsante.