Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Zaytun Seif Swai
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa wodi ya upasuaji ya wanawake na jengo la kuhifadhia maiti Hospitali ya Wilaya ya Karatu?
Supplementary Question 1
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi wa Karatu ninaishukuru Serikali kwa majibu hayo. Swali la kwanza; kwa kuwa, hospitali hii imejengwa sasa zaidi ya miaka miwili na huduma hii ya upasuaji kwa wanawake ni muhimu sana. Je, ni upi mkakati wa Serikali sasa, kuharakisha ujenzi wa wodi hii ya upasuaji kwa wanawake katika hospitali hii? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; hospitali ya Olturumet, Wilaya ya Arumeru ina changamoto kubwa ya ukuta na hii inahatarisha usalama wa wagonjwa na mali zao. Je, ni upi mkakati wa Serikali kujenga ukuta katika hiyo Hospitali ya Olturumet?  Ahsante. (Makofi)
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutambua umuhimu wa huduma za afya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepeleka fedha kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Halmashauri ya Karatu. Hospitali ile imejengwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema, Serikali inatambua kwamba bado kuna uhitaji wa wodi pamoja na jengo la upasuaji. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itaendelea kutenga fedha. Katika mwaka ujao wa fedha, Serikali imetenga milioni 800 kwa ajili ya kwenda kujenga jengo la upasuaji, wodi na njia za kupitia wagonjwa. Kwa hiyo, hatua hii tayari imeshachukuliwa Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Karatu, muwe na uhakika kwamba Serikali itakwenda kutekeleza mradi huo.
 
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusiana na Hospitali ya Olturumet katika Halmashauri ya Arumeru. Hospitali ile ni kongwe, lakini pia ilikuwa na uchakavu mkubwa sana wa majengo, Serikali ilipeleka zaidi ya shilingi milioni 900 mwaka wa fedha uliopita, imekarabatiwa na sasa inatoa huduma bora, lakini tunafahamu kuna uhitaji wa ukuta, tunaendelea kupanga bajeti zetu na tunajua tumeweka vipaumbele kwenye majengo ya huduma kwanza, lakini baadaye tutakuja kujenga pia kuta kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, usalama katika hospitali unakuwa mzuri zaidi. Ahsante.
							
 
											Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa wodi ya upasuaji ya wanawake na jengo la kuhifadhia maiti Hospitali ya Wilaya ya Karatu?
Supplementary Question 2
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi tunajenga Hospitali ya Halmashauri, lakini mtiririko wa fedha siyo mzuri majengo mengi hayajawa tayari. Je, Serikali ipo tayari sasa kuongeza speed ya kuleta fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ili tumalizie hospitali yetu ya wilaya? (Makofi)
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa hospitali za halmashauri zetu hufanywa kwa awamu. Tulianza na awamu ya kwanza katika ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na majengo yale yameshajengwa. Yapo ambayo yamekamilika na yapo ambayo yapo katika hatua za ukamilishaji, lakini nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutaendelea kutenga fedha kwenye bajeti za mwaka ujao ili kuhakikisha kwamba majengo yale yanakamilishwa mapema na kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi. Ahsante. (Makofi)
 
											Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa wodi ya upasuaji ya wanawake na jengo la kuhifadhia maiti Hospitali ya Wilaya ya Karatu?
Supplementary Question 3
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Tarafa ya Matamba ina Kata zaidi ya tano na katika Kata hizi tano hazina kituo cha afya hata kimoja, tunalazimika kupeleka maiti Wilaya ya Mbarali. Je, ni ipi kauli ya Serikali katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimkakati pale Matamba ili pawe na chumba cha kuhifadhia maiti? (Makofi)
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Tarafa ya Matamba katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete ni Tarafa kubwa, ina Kata ziadi ya tano, lakini haina kituo cha afya. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakumbuka Mheshimiwa Mbunge alishawasilisha Kata ya kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya. Nimhakikishie kwamba Serikali ipo hatua za mwisho za kupeleka fedha katika Tarafa ya Matamba kwa ajili ya ujenzi wa kile kituo cha afya ambacho kitakuwa ni miundombinu yote muhimu, ikiwemo jengo la kuhifadhia maiti ili kuhakikisha kwamba wananchi wetu hawapati usumbufu mkubwa wa kupeleka miili mbali na Halmashauri hiyo. Ahsante. (Makofi)
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved