Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Finance and Planning Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 107 2025-04-22

Name

Dorothy George Kilave

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa uzio kwa ajili ya ulinzi na usalama wa wanafunzi hususan maeneo ya mijini. Katika mwaka 2024/2025, Serikali ilitumia shilingi 190,735,794 kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika Shule za Msingi Wailes na Likwati na Shule za Sekondari Miburani na Nzasa zilizopo Manispaa ya Temeke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2025/2026, Serikali imepanga kutumia shilingi 200,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika Shule za Msingi Kibasila, Mji mpya na Kibondemaji na Shilingi 150,000,000 katika Shule mpya za Sekondari za Chang’ombe, Makangarawe na Mwembebamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha za ujenzi wa uzio katika shule za msingi na sekondari kupitia mapato ya ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kadri ya upatikanaji wa fedha.