Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dorothy George Kilave

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Supplementary Question 1

MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali je, mnaona kwamba chanzo kikubwa cha tabia mbaya za wanafunzi ni kutokana na kutokuwa na uzio kwa sababu huwa wanatoka na wakati mwingine vijana wengine wanapita tu katikati ya shule kwa sababu ya kutokuwa na uzio. Hamwoni sasa hata hizi shule zilizokuwa za zamani zipate uzio pamoja na hizi nilizotaja, lakini zipo nyingi ambazo zimebaki hazijajengewa uzio? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Je, hamwoni ipo haja sasa ya kutuma fedha au kutenga fedha katika shule mpya pamoja na fedha za uzio ili inapojengwa shule mpya na uzio uwepo? Ahsante. (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Dorothy Kilave, kwa kweli amekuwa akipaza sauti yake kuhakikisha kwamba Sekta ya Elimu katika Jimbo lake inaendelea kuimarika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie kwamba Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa uzio katika maeneo ya shule kwa sababu ya usalama, siyo tu wa wanafunzi pia mali za shule. Serikali imeshaanza kujenga uzio katika shule za zamani na shule mpya na itaendelea kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba maswali yake yote mawili nimjibu Mheshimiwa Mbunge kwa kumwambia kwamba Serikali tayari imeanza, inatenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhakikisha inafikia shule mbalimbali ambazo hazina uzio, inajenga uzio na itaendelea kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Supplementary Question 2

MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Sekondari ya Masonya ni Shule ya Wasichana na ipo katikati ya Kijiji cha Masonya. Shule ile haina uzio. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa uzio ili kuleta ulinzi na usalama kwa wanafunzi wale wa kike? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwanza kumpongeza Mheshimiwa Kungu kwa swali lake zuri kabisa kwa maslahi mapana ya Sekta ya Elimu na hasa katika Jimbo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie kwamba kupitia mapato ya ndani ya mamlaka zetu za Serikali za Mitaa tutatenga fedha na tutafika kwenye hii shule ya Masonya kwa ajili ya kuhakikisha kwamba uzio unajengwa ili kuweza kuimarisha usalama siyo tu wa wanafunzi bali wa mali hata za shule. (Makofi)

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Supplementary Question 3

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Shule ya Msingi Tukuyu inapakana na Kituo cha Polisi cha Tukuyu Wilayani Rungwe, haina uzio. Hii inaleta athari za kiakili kwa watoto wanapoona wahalifu wakipelekwa Polisi. Je, ni lini mtatoa fedha kwa ajili ya kujenga ukuta kutenganisha Kituo cha Polisi na hii Shule ya Msingi? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Sophia Mwakagenda kwa swali lake zuri kabisa ambalo linalenga kuimarisha usalama wa wanafunzi wetu wanapokuwa shuleni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na shule hii ya Tukuyu iliyopo Wilaya ya Rungwe, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri Serikali itafika katika shule hii ya Tukuyu kwa upekee ulioueleza wa kimazingira kuja kujenga uzio ili kutengeneza mazingira salama kabisa kwa ajili ya wanafunzi wetu katika shule hiyo. (Makofi)

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Supplementary Question 4

MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Sekondari ya Mbinga Girls ni shule pekee ya wasichana kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga. Wazazi kwa kutambua umuhimu wa ukuta wameanza kuchangisha na wameanza ujenzi. Je, ni lini Serikali itaunga mkono juhudi za wazazi wa Mbinga Girls? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Benaya Kapinag kwa kuuliza swali ambalo linalenga kuimarisha usalama wa wanafunzi wetu katika shule hii ya Mbinga Girls ambayo ipo katika Jimbo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa miundombinu hii ya uzio katika shule hizi kwa maana uzio huu unaendelea kuimarisha usalama wa wanafuzi wetu, pia usalama wa mali za shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie kwa sababu wananchi tayari wamehamasika na wameanza kutumia nguvu zao kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika hii shule hii ya Mbinga Girls, Serikali itafika haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kuja kuunga mkono jitihada hizi ili uzio huu uweze kukamilika na uweze kuwanufaisha wanafunzi wetu katika shule hii. (Makofi)

Name

Sebastian Simon Kapufi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Mjini

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Supplementary Question 5

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika Shule ya Mpanda Bay na Mwangaza, shule hizi zinapakana na makaburi. Ili kuwaepusha wanafunzi na sintofahamu ni lini Serikali itatuunga mkono kwa kutuongezea fedha? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Sebastian Kapufi kwa hili swali lake zuri kabisa ambalo linalenga kuimarisha Sekta ya Elimu katika Jimbo lake. Ninaomba nimhakikishie kwamba, Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa miundombinu ya uzio katika hizi shule zetu na hususan katika hii Shule ya Mbamba Bay pamoja na Mwangaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri itafika katika shule hizi kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za ujenzi wa uzio ili uweze kuwanufaisha wanafunzi wetu na shule ile kwa ujumla wake. (Makofi)

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Supplementary Question 6

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Bukoba Mjini, Shule ya Sekondari ya Wasichana Kagemu ya bweni ina zaidi ya watoto 730, haina uzio na kwa mazingira iliyopo inahitaji uzio kwa maana ya ukuta ili watoto wetu wa kike waendelee kuwa salama. Je, ni lini Serikali itatenga fedha ili kujenga uzio katika shule ya Sekondari ya Wasichana Kagemu iliyopo Bukoba Mjini? Ninashukuru. (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Neema Lugangira kwa hakika amekuwa ni Mbunge mchapakazi na swali lake hili limelenga kuboresha maslahi mapana ya Sekta ya Elimu katika Jimbo la Bukoba Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa uzio katika shule zetu hizi na hasa hizi za bweni. Nimhakikishie kwamba, Serikali itaunga mkono juhudi za ujenzi wa uzio katika hii shule aliyoitaja ili wanafunzi wetu waweze kupata mazingira salama zaidi ya kusomea pia kuimarisha ulinzi wa shule hii aliyoitaja. (Makofi)

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Supplementary Question 7

MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kwa kuwa Shule ya Msingi Ukombozi, Singida Mjini ipo katikati ya mji na haina uzio na ni chakavu sana. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kujenga uzio na kuikarabati shule hiyo? Ahsante.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Aysharose Mattembe kwa swali lake hili linalolenga kuboresha na kuimarisha Sekta ya Elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimfahamishe kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikitenga fedha kila mwaka wa bajeti kwa ajili ya kuendelea kuimarisha miundombinu katika upande wa Sekta ya Elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha miaka minne Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tayari amekarabati shule kongwe 906 zikiwemo za msingi na sekondari. Ninaomba nimhakikishie kwamba, Serikali itaendelea na jitihada hizo na itafika katika Shule hii ya Ukombozi kwa ajili ya kuikarabati pia kwa ajili ya kuhakikisha inajengewa uzio ili iweze kuwa na mazingira salama zaidi kwa ajili ya wanafunzi wetu kusomea na usalama wa mali za shule. (Makofi)

Name

Anne Kilango Malecela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Same Mashariki

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Supplementary Question 8

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri kwanza ninaishukuru sana Serikali kwa kutujengea shule nzuri sana ya kisasa inayoitwa Kalemawe Sekondari iliyopo ndani ya Kata ya Kalemawe. Shule hii ipo jirani sana na tembo wanapopitia kuelekea kwenye malisho yao, Mheshimiwa Waziri ninaomba uwaambie wananchi wale ni lini mtapeleka fedha za kujenga uzio kwa sababu tembo wale wamekuwa ni tatizo sana kwa wanafunzi na wakati mwingine wanafunzi wanaamua hata kutokwenda shule. Ninaomba uwajibu ili wakuelewe vizuri.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Anne Kilango Malecela kwa hili swali lake ambalo linalenga kuimarisha Sekta ya Elimu katika Jimbo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie kwamba tunaelewa mazingira haya hatarishi ambayo yapo katika shule hii ya Kalemawe na ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri aweze kuweka katika mipango na bajeti, fedha kwa ajili ya kuhakikisha shule hii inajengewa uzio ili iwe ina mazingira salama zaidi kwa ajili ya wanafunzi wetu kuweza kusomea. (Makofi)

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kutenga fedha za kujenga uzio katika Shule za Msingi na Sekondari – Temeke?

Supplementary Question 9

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Ninaipongeza Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga shule za wasichana katika mikoa yote. Sasa, ninataka kujua, ni nini mpango mkakati wa kuhakikisha kwamba, shule hizo kwa thamani kubwa ambayo zimejengwa zinakuwa na uzio au fence? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Omari Kigua kwa swali lake zuri, ambalo linalenga kuboresha na kuimarisha Sekta ya Elimu ya Sekondari. Ni kweli, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amejenga shule 26 za sayansi za bweni za wasichana, moja katika kila mkoa wa Tanzania Bara, kila moja ina thamani ya jumla ya shilingi bilioni 4.45. Shule hizi zimejengwa na ukamilifu wake wa kimiundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Serikali itahakikisha kwamba, kupitia mapato ya ndani, inafika katika shule hizi, kwa ajili ya kujenga uzio ili shule hizi ziwe zina mazingira salama zaidi, kwa ajili ya wanafunzi wetu. (Makofi)